KAMATI ya Usajili ya Yanga, imesitisha mpango wake wa kumsajili kiungo mshambuliaji mwenye kasi wa Villa SC ya Uganda, Emmanuel Okwi.
Tangu Simba imuuze mchezaji huyo kwa Watunisia hao Januari, mwaka huu kwa dau la dola 300,000 (Sh milioni 480), haijapata hata shilingi, hivyo suala la usajili wake bado lina mgogoro ambao umeshafikishwa Fifa ambayo imeidhinisha acheze URA kwa mkopo baada ya kugoma kuichezea Etoile kutokana na kutolipwa mishahara.
Chanzo cha habari cha uhakika kutoka ndani ya Yanga, kimeliambia Championi Jumatatu kuwa, uongozi unasubiri hadi matatizo ya usajili wake yatakapomalizika ndiyo uanze mchakato wa kuingia naye mkataba.
“Kiukweli Okwi alikuwepo kwenye orodha ya wachezaji tutakaowasajili kwenye usajili wa dirisha dogo, lakini imeshindikana kutokana na matatizo yake ya usajili kati yake na Fifa.
“Okwi alirudishwa Villa SC akiwa bado ana mkataba wa kuichezea Etoile, hivyo hapo ndiyo tunapata ugumu,” kilisema chanzo hicho.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Abdallah Bin Kleb, alisema: “Tunafanya usajili kwa mujibu wa ripoti ya kocha ambayo tunaendelea kuifanyia kazi, hayo mengine yatafuata baadaye.”






