STAA wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ amesema alipata wakati mgumu kumpanga mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwenye filamu yake ambayo walipaswa kucheza kama wapenzi kwa kuhofia kumbusu.
Vincent Kigosi ‘Ray’.
“Lulu alikuwa na uwezo wa kumudu kipengele hicho, kipindi hicho alikuwa mdogo sana, niliona ni jambo la aibu kidogo kumbusu mdomoni mtoto mdogo kama yeye halafu ni kitu ambacho jamii itakaa ikitazame nikaona bora nimchukue Nagris, Lulu nikampa sini nyingine,” alisema Ray.Aliongeza kuwa, kikubwa kilichomfanya avutiwe kucheza na Nagris ni kwa sababu ni mwanamke ambaye katulia na hana skendo hivyo itamuongezea heshima na mvuto wa kazi yake katika jamii.






