Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts

FIFA YATOA ORODHA YA UBORA KISOKA, TANZANIA YAZIDI KUDIDIMIA


Timu ya taifa ya Wales, imeandika historia mpya baada shirikisho la soka duniani FIFA, kutoa orodha ya viwnago vya ubora wa soka vya mwezi huu kwa kuzingatia vigezo vya michezo ya kimataifa iliyochezwa siku za hivi karibuni.

Wales wameandiaha historia hiyo baada ya miaka 20 kupita ambapo wameonekana kukwea kwa nafasi 12 na kufanikiwa kuwakamata ndugu zao Sotland katika nafasi ya 29.
Mafanikio ya kupanda katika viwango hivyo vya ubora duniani yametokana na ushindi wa mabao 2-1 ulioshuhudia Wales wakiinyanyasa Andorra katika harakati za kuwania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka 2016.
Kwa upande wa timu ya taifa ya Ireland ya Kaskazini imechupa kwa nafasi 24 na kukamata nafasi ya 71 ikiwa ni nafasi tisa nyuma ya Jamuhuri ya Ireland.
Timu ya taifa ya Uingereza imepanda kwa nafasi mbili ikitoka katika nafasi ya 20 hadi katika nafasi ya 18.
Jamuhuri ya Ireland imepanda katika viwango vya ubora kufuatia ushindi wao wa kwanza wa mabao 2-1 wakati wa kampeni za kusaka tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya dhidi Hungary, ili hali timu ya taifa ya Uingereza iliichabanga Uswiz mabao 2-0.
Mabingwa wa soka duniani timu ya taifa ya Ujerumani, imeendelea kusalia katika nafasi ya kwanza, kufuatia ushindi wa mabao mawili kwa moja walioupata dhidi ya Scotland walipoanza kampeni ya kuelekea nchini Ufaransa mwaka 2016.
Hata hivyo kabla ya mchezo huo, Ujerumani waliambulia kisago cha mabao manne kwa mawili mwanzoni mwa mwezi huu, kutoka kwa Argentina lakini haikuharibu mpango wa kuendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa viwango vya ubora wa soka duniani.
Timu ya taifa ya Colombia nayo imepanda kwa nafasi tatu, ikiziacha timu za taifa za Uholanzi, Ubelgiji, Brazil, Uruguay, Hispania, Ufaransa pamoja na Uswiz zinazotengeneza orodha ya kumi bora.
Orodha kamili ya viwango vya ubora wa soka duniani ambavyo vimetolewa hii leo na shirikisho la soka duniani FIFA Bofya Hapa

PICHA 11 ZA WANAMICHEZO MAARUFU JINSI WALIVYOKUWA UTOTONI NA SASA, HUWEZI AMINI, ZIANGALIE HAPA

6Messi
0

Wengi kati yao sura zao hazijabadirika sana tangu kipindi chao cha utotoni lakini picha hizi zitakuonyesha kwamba wanamichezo hawa wameanza kucheza michezo yao tangu wakiwa watoto.Kwenye picha hizi kuna watu kama Cristiano Ronaldo,Lebron James,Lewis Hamilton,Tiger Woods,Michael Owen na wengine.
1Neymar
2David Beckham
3Michael Owen
4Lewis Hamilton
5Diego Maradona
7Lebron James
8Tiger Woods
9Serena na Venus Williams
10

KAMA JANA ULIPITWA, HII NDIO HIGHLIGHT YA MECHI ZA FA CUP


Wilfried Bony wa Swansea baada ya kufunga bao la pili na la ushindi dhidi ya Manchester United.
Mchezaji wa Manchester United, Danny Welbeck, akiwa kichwa chini miguu juu wakati wa mtanange huo uliomalizika kwa Swansea kushinda 2-1.
Manchester United 1-2 Swansea City
Liverpool 2 - 0 Oldham Athletic
Derby County 0 - 2 Chelsea
Sunderland 3 - 1 Carlisle United
Nottingham Forest 5 - 0 West Ham United




Derby County 0 - 2 Chelsea- all goals
All Goals FA Cup - Manchester United 1 - 2.
FA Cup - Liverpool 2-0 Oldham (Highlights) 05.

LEWANDOWSKI ASAINI MKATABA MPYA NA BUYERN MUNICH BUREE

Klabu ya Bayern Munich hatimaye imethibitisha kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Poland Robert Lewandowski .Lewandowski amesaini mkataba wa miaka mitano ambapo ataanza kuichezea Bayern Munich mwezi julai mwaka huu baada ya kuisha kwa msimu wa sasa wa ligi ya Ujerumani ambako atakuwa anamalizia mkataba wake na Borrusia Dortmund. Robert Lewandowski anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya na klabu ya Bayern Munich baada ya kusaini ikiwa ni taratibu za mwisho kabla ya kujiunga nayo rasmi.
Lewandowski yuko kwenye miezi sita ya mwisho ya mkataba wake na Dortmund hali inayomruhusu kuingia makubaliano ya awali na klabu nyingine na atajiunga na Bayern kuanzia msimu ujao ambapo anaondoka Dortmund bure.

TURKISH AIRLINE LAMPANDISHA MESSI MLIMA KILIMANJAROmi

YANGA KWANUKA, YATIMUA BENCHI LAKE LOTE LA UFUNDI, SOMA ZAIDI HAPA

ufundi
Klabu bingwa ya soka Tanzania, Yanga imetimua benchi lake lote la ufundi kwa kile kilichoelezwa kuwa kushindwa kuleta matunda yaliyokusudiwa katika klabu hiyo.

Kutokana na hatua hiyo, Yanga imetangaza kujitoa katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi yanayoanza leo huko Zanzibar.

Katibu Mkuu wa Yanga, Benno Njovu alisema jana kuwa klabu yake imechukua hatua hiyo ili kujipanga upya kwa michuano ya kimataifa pamoja na Ligi Kuu Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza wiki tatu zijazo.

Msemaji wa Kombe la Mapinduzi, Farouq Karim alielezea kusikitishwa na hatua ya Yanga kujitoa katika michuano hiyo na kusema Ashanti ya Ilala imechukua nafasi ya timu hiyo.

Njovu alisema kuwa kutokana na kupewa notisi ya kutimuliwa; Kocha Msaidizi; Fred Felix “Minziro”, Kocha wa Makipa; Razak Siwa na Daktari wa Timu, Nassoro Matuzya, kwa sasa Yanga haina kiongozi wa benchi la ufundi.

Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandits alikwishatupiwa virago kwa kupewa notisi ya mwezi mmoja, siku chache baada ya kufungwa na Simba mabao 3-1 katika mechi ya Mtani Jembe kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza jana, Siwa alisema: “Nakubaliana na uamuzi wa viongozi, siwezi kubishana nao kwa kuwa wao ndiyo wenye uamuzi wa mwisho kuhusiana na klabu.”

Njovu alisema kuwa kwa sasa uongozi unaendelea na mchakato wa kuwapata warithi watakaochukua nafasi hizo haraka ili waweze kuanza maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika baadaye Februari.

Yanga imepangwa kuanza ugenini na Komorozine ya Comoro kwa mechi za kwanza zitakazoanza kuchezwa kati ya Februari 7 na 9, mwaka huu.

Hata hivyo, Njovu alisema kuwa hadi kufikia jana, makocha 45 wametuma maombi ya kutaka kuinoa Yanga.

Simba uwanjani leo

Wakati hayo yakitokea Jangwani, Simba leo inashuka kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar kupambana na AFC Leopards ya Kenya katika mchezo wake wa kwanza wa Kombe la Mapinduzi huku mgeni rasmi akiwa Kocha wa Mkuu wa Timu ya Taifa ya Italia, Cesare Prandelli.
Michuano ya Kombe la Mapinduzi ni sehemu ya maandalizi ya sherehe za kutimiza miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar na mwaka huu itashirikisha timu 12.
Mchezo huo wa Simba na Leopards utakaoanza saa 2:00 usiku, utatanguliwa na ule wa wenyeji KMKM ya Zanzibar ambayo itashuka kwenye uwanja huohuo, saa 10:00 jioni kuikabili KCC ya Uganda ikiwa ni mechi za Kundi A.
Mechi nyingine leo jioni kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba, itazikutanisha Mbeya City na wenyeji Cloves Stars, ambayo ni kombaini ya Kisiwa cha Pemba.
Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Selemani Matola alisema jana kuwa kikosi chake kimejiandaa vizuri na matarajio ya kufanya vizuri leo.
“Timu yangu ipo tayari kwa mechi ya kwanza na kwa mazoezi tuliyofanya naamini tutaifunga Leopards na kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele japokuwa tunaweza kukutana na ugumu, maana kama unavyoona kuna timu kutoka nje ya nchi hapa,” alisema Matola.
Naye beki wa Simba, Donald Mosoti ‘Musso’ alisema atahakikisha anawakaba vilivyo washambuliaji wa AFC Leopards, Allan Wanga na Jacob Kelly leo.

—MWANANCHI—

KOCHA WA MAN UTD ANYIMWA HELA ZA USAJILI KWENYE DIRISHA DOGO LA USAJILI


Kocha wa Man United, David Moyes
KLABU ya Manchester United inahofia jitihada zake za beki mpya wa kushoto katika usajili wa dirisha dogo Januari hauwezi kuvunja matunda, kwa Everton na Southampton kutokuwa na mpango wa kuwaachia wachezaji wake Leighton Baines na Luke Shaw.
Kocha wa United, David Moyes alijaribu bila mafanikio kutaka kumsaini Baines kutoka klabu yake ya zamani mapema msimu huu, baada ya Patrice Evra kusema anahitaji ushindani wa maana wa namba katika nafasi yake.
Lakini juhudi za United zimezimwa na Mwenyekiti wa Everton, Bill Kenwright na pamoja na hayo Moyes ameambiwa na Mtendaji Mkuu wa klabu yake, Ed Woodward kwamba hana fedha za kutoa kwa ajili ya usajili wa mwezi ujao.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England wanahofia watakutana na mazingira yale yale kutoka klabu ya Merseyside, pamoja na Southampton juu ya Shaw wanayemtaka.
Shaw, mwenye umri wa miaka 18, pia yupo kwenye rada za Chelsea, lakini Southampton imeweka wazi kwamba haimuuzi mchezaji huyo.
United inahaha kusaka beki wa kushoto kutokana pia na Mholanzi, Alexander Buttner kushindwa kufanya vizuri tangu asajiliwe na Sir Alex Ferguson mwaka 2012.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, binafsi anatakiwa na Tottenham katika usajili huu wa Januari, ameanza katika mchezo mmoja tu wa Ligi Kuu msimu huu, maana yake kwamba Evra, akiwa na umri wa miaka 32, amebeba majukumu makubwa ya timu katika nafasi hiyo.
Tayari msimu huu, beki huyo wa Ufaransa amecheza mechi 29 za klabu yake na hi yake katika mashindano yote. Chanzo: binzubeiry
A

MICHAEL SCHUMACHER AMBAYE NI BINGWA WA MBIO ZA MAGARI MAARUFU HALI YAKE MAHUTUTI HOSPITALINI

GRENOBLE, France — Doctors treating Michael Schumacher refused Monday to predict an outcome for the seven-time Formula One champion, saying they were taking his critical head injury "hour by hour" following a skiing accident.
Chief anesthesiologist Dr. Jean-Francois Payen told reporters that Schumacher was still in a medically induced coma and doctors were focusing only on his current condition.
"We cannot predict the future for Michael Schumacher," said Payen, who is also in charge of Grenoble University Hospital's intensive-care unit.
"He is in a critical state in terms of cerebral resuscitation," he added. "We are working hour by hour."
Schumacher, the most successful driver in Formula One history, arrived at the Grenoble hospital a day earlier, already in a coma, and immediately underwent brain surgery.
The German driver was skiing with his son Sunday morning in the French Alpine resort of Meribel when he fell and hit the right side of his head on a rock. He was wearing a helmet, but doctors said it was not enough to prevent a serious brain injury. Payen said Schumacher would have died without the helmet.
Gerard Saillant, a trauma surgeon who operated on Schumacher when he broke his leg in a 1999 race crash, was at the hospital as a visitor. He told reporters that Schumacher's age — he turns 45 on Jan. 3 — and his fitness should work in his favor.
But the Grenoble medical team was cautious about Schumacher's prognosis.
They lowered his body temperature to between 34 and 35 degrees Celsius (93.2 to 95 degrees Fahrenheit) as part of the medically induced coma, which essentially rests the brain, slowing its metabolism to help reduce inflammation after an injury.
The neurology team at Grenoble University Hospital is recognized as among the best in France and the hospital, in a city that is the gateway to the French Alps, sees a large number of skiing accidents every year.
Schumacher has been seriously hurt before. In addition to the broken leg in a crash at the Silverstone race course, he also suffered serious neck and spine injuries after a motorcycle accident in February 2009 in Spain.
The area where Schumacher was skiing is part of a web of trails that slice down through a vast and, in parts, very steep snowfield. Although challenging, the snowfield is not extreme skiing. The runs are broad and neatly tended, and the ungroomed area in between, known as off-piste — where the resort said Schumacher was found — is free of trees.
The resort said Schumacher was conscious when first responders arrived, although agitated and in shock. But Payen said Monday that after the fall Schumacher was not in a "normal state of consciousness." He was not responding to questions and his limbs appeared to move involuntarily.
He was airlifted to a local hospital and then later brought to Grenoble. Doctors said that stopover was typical and did not affect his condition.
His wife and other family members were at his bedside.
"The family is not doing very well obviously. They are shocked," said his manager Sabine Kehm, who added that the family still appreciated the outpouring of support.
The French prosecutor in Albertville has opened an investigation into the accident, according to the Mountain Gendarmerie in Bourg-Saint-Maurice, which will participate in the probe. The goal is to determine the circumstances of the accident and what was responsible for it.
Formula One drivers and fans rushed to wish Schumacher a quick recovery.
"Like millions of Germans, the chancellor and members of the government were extremely dismayed when they heard about Michael Schumacher's serious skiing accident," German Chancellor Angela Merkel's spokesman, Steffen Seibert, said in Berlin.
Sebastian Vettel, for whom Schumacher was a boyhood idol, told German news agency dpa: "I am shocked and hope that he will get better as soon as possible."
Ferrari, which Schumacher raced for, expressed its concern in a statement.
"Everyone at Ferrari has been in a state of anxiety since hearing about Michael Schumacher's accident," it said, adding that company president, Luca di Montezemolo, and race team leader, Stefano Domenicali, were in contact with the family.
British former world racing champion Jenson Button said posted that his "thoughts are with Michael Schumacher at this tough time. ... Michael more than anyone has the strength to pull through this."
During his career, Schumacher won seven drivers' championships and 91 race wins. After initial success with the Benetton team, Schumacher moved to Ferrari and helped turn the Italian team into the sport's dominant force. After initially retiring in 2006, he made a comeback in 2010 and raced for three years with Mercedes.

MABASI YATUMIWAYO NA KLABU KUBWA ZA ULAYA SASA KUTUMIWA NA AZAM FC,NDANI LINA TV KILA SITI, CHOO NA FRIJI, LAINGALIE HAPA



Hakuna Afrika nzima; Basi jipya la wachezaji wa klabu ya Azam FC ya Dar es Salaam, lililowasili nchini juzi likiwa tayari kusafirishwa visiwani Zanzibar ambako timu hiyo imekwenda kushiriki Kombe la Mapinduzi. Hili ni aina ya mabasi ambayo yanatumiwa na klabu za Ulaya kama Manchester United, Bayen Munich na Barcelona ambalo kwa Afrika Azam inaweza kuwa klabu ya kwanza kulimiliki.
Kitu cha maana
Kila siti ina TV
Kuna friji

LEO NI MECHI KATI YA SIMBA NA YANGA, NANI MKALI ZAIDI, KILA KITU KUJULIKANA LEO

Mashabiki wa timu ya Yanga Fc.
WATANI wa jadi katika soka nchini, timu za Yanga na Simba, leo zinashuka katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuhitimisha majigambo ya ‘Nani Mtani Jembe’ baina yao katika mechi kali inayofanyika chini ya uratibu wa mdhamini wao, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).                                             Mashabiki wa timu ya Simba Fc.
Mbali ya wapenzi na mashabiki wa timu hizo kusubiri kuona ‘nani mtani jembe’ kati yao, pia watapata fursa ya kushuhudia nyota wapya waliosajiliwa kupitia dirisha dogo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mkuu na Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema maandalizi ya mechi hiyo ya aina yake yamekamilika.

Wambura alisema vikosi vya ulinzi na usalama katika mechi ya leo vimekamilika kila idara na kwamba Barabara ya Taifa inayoanzia Keko-Maghorofani hadi Barabara ya Mandela, itafungwa kuanzia saa 12 asubuhi kupisha hekaheka za mtifuano huo.

Alisema magari hayataruhusiwa kuegeshwa kuanzia eneo la Baa ya Minazini hadi msikiti unaotazamana na Uwanja wa Uhuru, hivyo magari yote yataegeshwa nje ya Uwanja wa Ndani wa Taifa – kando ya Barabara ya Mandela.

“Magari yatakayoruhusiwa kuingia maeneo hayo na hata ndani ya Uwanja wa Taifa ni yatakayokuwa na stika zilizotolewa na TFF. Tunawaomba wadau na mashabiki wa soka kuheshimu na kutii maagizo ya vikosi vya ulinzi,” alisema Wambura.

Aliongeza kuwa milango ya kuingilia uwanjani itakuwa wazi kuanzia saa sita mchana ambapo baada ya mauzo ya tiketi ya jana, zoezi hilo litaendelea leo nje ya uwanja huo kabla ya mechi ili kuwapa mashabiki fursa ya kukata na kuingia moja kwa moja.

Pambano la leo linasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka wanaohitaji sio tu kuona nyota wapya waliosajiliwa na klabu hizo, pia kujua ‘nani jembe’ ndani ya uwanja kwani kwa nje ya uwanja, Yanga ni kama imeshinda kutokana na kuwa kwenye mazingira mazuri kisaikolojia.

Nje ya uwanja, Nani Mtani Jembe ilihusisha vita baina ya mashabiki wa kila klabu ‘kupora’ mamilioni ya mwingine kupitia shindano la kinywaji cha Kilimanjaro Premium Lager ambapo Simba ilizidiwa na Yanga kwa kiasi kikubwa cha pesa.

Ukiondoa shangwe ya mashabiki wa Yanga kumpata mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi akitokea SC Villa ya Uganda na Juma Kaseja, Simba leo itakuwa na makipa waliowahi kudaka Jangwani kwa vipindi tofauti, Ivo Mapunda na Yaw Berko.

Nyuma ya majina hayo makubwa, Yanga ilinasa saini ya kiungo Hassan Dilunga kutoka Ruvu Shooting ya Pwani, wakati Simba iliwasainisha kwa mpigo kiungo mchezeshaji Awadh Juma Issa kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro na Ally Badru Ally kutoka Canal Suez ya Misri.

Kila timu ilishajichimbia kambini kunoa makucha kuelekea pambano hilo ili kusawazisha makosa yaliyowafanya watani hao kutoka sare ya 3-3 katika mechi ya raundi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa Oktoba 20.

Uwepo wa nyota wapya kwa kila upande ambao watashirikiana na wakali wengine, unalifanya pambano la leo liwe lenye mvuto wa aina yake ambapo kiingilio cha chini ni sh 5,000 kwa viti vya kijani.

Kwa upande wa viti vya rangi ya bluu, kiingilio ni sh 7,000; viti vya rangi ya chungwa sh 10,000; VIP C ni sh 15,000; VIP B sh 20,000 huku VIP A sh 40,000.

Kwa upande wa waamuzi, kati atasimama Ramadhan Ibada ‘Kibo’ wa Zanzibar, atakayesaidiwa na Ferdinand Chacha wa Bukoba na Simon Charles wa Dodoma huku Israel Nkongo wa Dar es Salaam akiwa mezani. Kazi ya kutathimini utendaji wa waamuzi wote itakuwa chini ya Soud Abdi wa Arusha.

MECHI TANGU 2010

Rekodi ya watani hawa inaonyesha kuwa mechi ya leo ni ya tisa tangu mwaka 2010 na katika mechi nane, Yanga imeshinda tatu, Simba mbili na wamekwenda sare tatu.

Aprili 18, 2010: Simba 4, Yanga 3

Oktoba 16, 2010: Yanga 1, Simba 0

Machi 5, 2011: Yanga 1, Simba 1

Oktoba 29, 2011: Yanga 1, Simba 0

Mei 6, 2012:  Simba 5, Yanga 0

Oktoba 3, 2012: Yanga 1, Simba 1

Mei 18, 2013: Yanga 2, Simba 0

Oktoba 20, 2013: Simba 3, Yanga 3

OKWI KWENDA YANGA, RAGE ASEMA WAKULAUMIWA SI YEYE, SOMA HAPA KUMJUA

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage ameibuka na kusema kuwa lawama za kutokumsajili mshambuliaji wao wa zamani kutoka Uganda, Emmanuel Okwi zielekezwe kwa Kamati ya Usajili na Ufundi wa timu hiyo na wala siyo yeye.

Rage ambaye alikuwa nchini Marekani kwa mwezi mmoja akimuuguza mwanaye, alisisitiza kuwa Okwi alikwishauzwa kwa timu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia na wala hakuwa wa Simba tena pamoja na wao kuendelea kudai fedha zao.

Alisema kuwa wakati anakwenda kumuuguza mwanaye, alikuwa amefanikiwa kusajili wachezaji wawili, Awadh Juma na Badru Ali tu, lakini huku nyuma bila ya kupata baraka zake, Kamati ya Usajili ilifanikiwa kumpa mkataba kocha mpya, Zdravko Logarusic kutoka Croatia na kusajili wachezaji watatu, makipa, Yaw Berko, na Ivo Mapunda na mlinzi Mkenya, Donald Musoti.

“Ikumbukwe kuwa Okwi alikuwa anakuja mara kwa mara hapa nchini, lakini kamati hizo hazikuona umuhimu wake, hawakufanya naye mazungumzo kujua nini kinachoendelea kuhusiana na timu yake ya Tunisia na sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kutaka kunichafua mimi na kuonekana mbaya na adui kwa klabu ya Simba,” alisema Rage.

Alisema kuwa kilichokuwa kinazungumzwa muda wote ni kunitaka mimi kujiuzulu na kuwaachia madaraka, jambo ambalo haliwezekani kwani lazima wajue kuwa mimi ndiye mkombozi wa Simba.

“Nimefanya mabadiliko makubwa, kuanzia kuongeza kodi ya mapango yetu na klabu kuingiza fedha, kutoka kodi ya Sh200,000 mpaka sasa ya mamilioni, sasa watu wanataka kuona fedha hizo zinapotea na kuwatumia watu ili niondoke, nasema hili halitawezekana na kwa taarifa tu, wale wenye mipango ya kunivamia nyumbani, nimekwisha toa taarifa polisi na hatua kali watachukuliwa wakithubutu kufanya hivyo,” alisema.

Alisema kuwa njama nyingi zimefanyika katika suala la Okwi mpaka kujiunga na Yanga, lakini kwa sasa yeye anasimamia zaidi suala la malipo ya timu ya Etoile na mchakato huo unakwenda vizuri.

 “Hivi leo Mbwana Samatta akijiunga na Yanga au Azam FC, watanilaumu mimi, Okwi hakuwa mchezaji wetu, wana-Simba wajue hilo, kuzungumzia suala la Okwi na kunishutumu mimi ni kunionea tu, walipaswa kujua suala la fedha, nalo nimelizungumza sana na kutoa ufafanuzi, lakini kwa vile lengo lao mimi niondoke, wanaongea maneno mengi ya uzushi juu yangu… mimi ni kiongozi mwenye sifa na kujua mambo ya uongozi, siwezi kukurupuka kujibu suala lolote,” alisema.

Alisema kuwa suala la malipo ya Okwi siyo siri, kwani Kamati ya Utendaji inaelewa kuwa tumefungua kesi Fifa na kulipa Dola 10,000 ili malalamiko yetu yapangiwe jaji na kusikilizwa.

“Kuna barua ililetwa na Fifa kwa njia ya DHL, ilifika klabuni muda mrefu, barua hiyo ilikuwa na majibu ya Fifa na njia gani tufuate ili tuweze kupata haki yetu ya Dola 300,000 za Marekani, makusudi haikutiliwa mkazo, leo (jana) nimefanikiwa kulipa Dola 10,000 kutoka mfukoni mwangu na tunasubiri kusikilizwa kwa madai yetu,” alisema.

KILIMANJARO STARS YAFUNGWA KWENYE KUTAFUTA MSHINDI WA NAFASI YA 3 YA CECAFA

Timu ya taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ imeshika nafasi ya nne michuano ya Kombe la CECAFA 2013 inayofanyika nchini Kenya baada ya kufungwa na timu ya Zambia kwa penalti 6-5.

Mchezo huo uliokuwa wa kutafuta mshindi wa tatu wa kombe hilo ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo bao la Zambia lilifungwa na Ronald Kampamba katika dakika ya 51 na Kilimanjaro Stars ilisawazisha kupitia kwa Mbwana Samatta katika dakika ya 65 kipindi cha pili ambapo dakika 90 ziliisha kwa sare ya bao 1-1.

Wachezaji wa Kilimanjaro Stars waliopata penalti ni Mbwana Samatta, Erasto Nyoni, Himid Mao, Amri Kiemba na Ramadhan Singano ‘Messi na waliokosa ni Haruna Chanongo, Mrisho Ngassa na Kelvin Yondani.

MANJI AJIWEKA PEMBENI NA MAJUKUMU YA CLUB YA YANGA

Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji.

MWENYEKITI wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji, ametangaza rasmi kutowania tena nafasi ya uenyekiti kwenye uchaguzi mkuu wa klabu hiyo utakaotangazwa baadaye mwakani.
Manji alichukua wadhifa huo mwaka jana baada ya kuondolewa kwa aliyekuwa Mwenyekiti, Lloyd Nchunga, aliyekuwa amebakiza miaka miwili ya uongozi wake klabuni hapo.
Manji ambaye pia ni mfadhili wa klabu hiyo alitoa tamko juu ya nia yake hiyo jana kwenye makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo Jangwani, Kariakoo jijini Dar es Salaam huku akitoa sababu kuwa ni kuwapisha wengine wenye uwezo wa kuiongoza timu hiyo nao kuchukua jahazi.
Amesema ametangaza kutowania nafasi hiyo mapema ili kuwapa nafasi nzuri wanaotaka kufanya hivyo wajipange mapema.
“Sitagombea tena uenyekiti kwenye uchaguzi ujao, nitawaachia wengine waendeleze hapa nilipoishia mimi, nimetangaza mapema ili wanaoitaka hii nafasi wajipange, maana wapo wenye nia lakini wanahofia kuchuana na mimi.
“Ninaweza kugombea lakini si sasa labda baadaye na siyo uchaguzi huu, nitafikiria kwanza kabla ya maamuzi hayo,” alisema Manji.
Kiongozi huyo aliongeza kuwa ataendelea kuiongoza Yanga kwa miezi saba iliyosalia.
Aidha, alisema kuwa bado tarehe rasmi ya uchaguzi huo haijafahamika na kudai kuwa itajulikana mara baada ya Mkutano Mkuu wa Yanga utakaofanyika Januari 19, mwakani.
“Nikishajitoa rasmi kwenye madaraka ya uongozi wa Yanga baada ya kuwa nimemaliza muda wangu nitaendelea kuwa shabiki wa kawaida wa Yanga kama ilivyo kwa wengine na kuhusu udhamini litabaki kuwa suala la klabu kuchagua mdhamini wao,” alisema Manji.

STARS ITATOKWA KWELI DHIDI YA KENYA INAYOBEBWA KAMA MTOTO NA MAREFA KWENYE NUSU FAINALI YA MICHUANO YA CHALLENGE?


15_837f7.jpg
Mungu Ibariki Tanzania: Kikosi cha Stars Challenge 2013 na chini ni Harambee....na "Washindwe".
KENYA_d7b78.jpg
Na Mahmoud Zubeiry, Machakos
TANZANIA Bara 'Kilimanjaro Stars', leo inashuka dimbani kwenye Uwanja wa Kenyatta, Machakos, kumenyana na wenyeji, Kenya 'Harambee Stars' katika Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge kuanzia saa 7:00 mchana.
Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Stars chini ya kocha Mdenmark, Kim Poulsen kufika Nusu Fainali ya michuano hiyo, baada ya mwaka jana pia mjini Kampala, Uganda ambako ilitolewa na wenyeji, Uganda 'The Cranes' kwa kufungwa mabao 3-0.(P.T)
Lakini Kim, amelipa kisasi kwa The Cranes, baada ya Stars kuivua ubingwa Uganda Jumamosi kwa kuitoa kwenye Robo Fainali, Uwanja wa County ya Mombasa, zamani Manispaa kwa penalti 3-2, kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90.
Baada ya kumaliza shughuli hiyo pevu, Kim anakabiliwa na jukumu lingine zito mbele yake, ambalo ni Nusu Fainali dhidi ya Kenya, ambayo imeonekana 'kubebwa' mno na marefa hadi sasa katika mashindano haya.
Kenya imekuwa ikipewa penalti katika mechi zote kuanzia hatua ya makundi hadi Robo Fainali na hali hiyo inatarajiwa kwa kiasi kikubwa kuendelea na leo pia Machakos.
Beki wa Azam FC, Joackins Atudo amepiga penalti nne na kufunga tatu hadi sasa, wakati moja alikosa katika mechi ya Kundi A dhidi ya Sudan Kusini.
Habari njema ni kwamba, kipa wa Stars, Ivo Mapunda anaheshimika mno kwa uhodari wa kucheza penalti, lakini pia Wakenya wanamuamini mno Atudo katika upigaji.
Mechi hiyo imeteka hisia za wengi na sababu za Shirikisho la Soka Kenya (FKF) kuipeleka Uwanja wa Kenyatta badala ya Nyayo, Nairobi ni kutokana na imani kwamba watu wa huko huishagilia mno Harambee Stars inapocheza.
Wakati Stars iliitoa Uganda, Kenya waliingia Nusu Fainali baada ya kuifunga 1-0 Rwanda 'Amavubi' kwa bao la penalti iliyotolewa katika mazingira ya utata iliyopigwa na Atudo kama kawaida.
Kenya ina ukuta imara, safu nzuri ya kiungo, lakini haina makali sana katika safu yake ya ushambuliaji, wakati Tanzania Bara japokuwa itamkosa kiungo wake, Salum Abubakar 'Sure Boy' aliyeonyeshwa kadi nyekundu dhidi ya Uganda, bado ina viungo wengine bora wa kuziba pengo hilo.
Kuna chipukizi Hassan Dilunga wa Ruvu Shooting na mkongwe Athumani Iddi 'Chuji' wa Yanga, ambao yeyote kati yao Kim anaweza kumpa jukumu la kuziba pengo la kiungo wa Azam FC, Sure Boy.
Stars ina ukuta imara kama ilivyo kwa safu ya kiungo na utamu zaidi ni safu yake ya ushambuliaji inayoundwa na wakali wawili wa TP Mazembe ya DRC, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu kwa pamoja na Mrisho Khalfan Ngassa wa Yanga.

Iwapo hali ya Ngassa haitakuwa imeimarika, hakuna shaka 'viberenge' vya Simba SC, Haroun Chanongo na Ramadhani Singano 'Messi' mmoja wao anaweza kuchukua nafasi na akafanya kazi nzuri- lakini pia kuna makinda mengine mawili ya Azam FC, Joseph Kimwaga na Farid Mussa pia wanaweza kucheza nafasi hiyo.
Litakuwa pengo kumkosa Ngassa kutokana na uzoefu wake ambao tayari anao hivi sasa kisoka, lakini pia itakuwa nafasi nzuri kwa chipukizi hao kuupambanua uwezo wao, iwapo watapewa nafasi.

Himid Mao amemaliza adhabu ya kadi na baada ya kuwa nje ya Uwanja katika mechi dhidi ya Uganda, leo anarudi kwenye mashindano na litakuwa jukumu la Kim kumchezesha kiraka huyo wa Azam, au kumpanga tena Michael Aidan wa Ruvu Shooting. Nusu Fainali nyingine ni kati ya Zambia na Sudan mjini Mombasa. Kila la heri Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars'.