BAADA ya watanzania kumwandama Ommy Dimpoz kutokana na tusi alomtukana marehemu Albert Mangwea, msanii huyo ameamua kuwapigia magoti watanzania na kuwasihi wamsamehe.
Hali hiyo imekuuja baada ya watu mbalimbali kutangaza kumsaka Ommy kwa lengo la kumwadabisha kwa kumpa kichapo kikali.
Miongoni mwa watu hao ni TID ambaye jana kupitia ukurasa wake wa facebook ametangaza vita dhiti ya Ommy Dimpoz.
Hii ni post ya Ommy ambayo ameitoa akiomba asamehewe kwa kauli zake na matusi aliyoyatoa kwa marehemu Ngwea.

Samahani tena sana na sitawacha kuomba msamaha, nimekubali makosa na hivi sasa naelekea nyumbani kwao kuomba msamaha kwa familia na nitue kwa vituo vya radio kuomba msamaha kwa wabongo na wote niliowaudhi. Samahani sana na nakubali mimi si mtu bila nyinyi na sikuongea kuhusu legend Ngweir kwa ila mbaya. One love