ANT EZEKIEL AENDELEZA UMALAYA WAKE, WANASWA AKIWA KIMAHABA NA KASSIM NCHINI MAREKANI

Wakati mumewe Sunday Demonte akidaiwa kuwa yuko mbioni kuhukumiwa kwenda jela huko Dubai, staa wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel Grayson amenaswa laivu kimahaba nchini Marekani akiwa na msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Kassim Mganga.

Staa wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel Grayson amenaswa laivu kimahaba nchini Marekani akiwa na msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Kassim Mganga.
Wakati anaondoka nchini hivi karibuni, Aunt alionekana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar, akiwa na mwanaume ambaye anadaiwa kuwa ni mume wa mtu, Moses Iyobo ‘Moze’.Baada ya habari hiyo kuripotiwa na gazeti tumbo moja na hili, Ijumaa Wikienda, Septemba 15, mwaka huu, ilidaiwa kwamba ndugu wa mumewe, Sunday hawakufurahishwa na kitendo hicho.
Wakipata msosi.
“Tunashangaa kumuona Aunt ameambatana na mume wa mtu na huko anakoenda pia tunasikia watakuwa wawili tu na Kassim, inatutia shaka kwa kweli,” alisema mmoja wa ndugu wa mume kwa sharti la kutoanika jina lake.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichopo nchini Marekani, wawili hao walitia maguu hivi karibuni kwa mwaliko maalum wa Ubalozi wa Tanzania nchini humo ambapo Kassim alipewa nafasi mbili hivyo akaamua kumchukua Aunt.
Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Kassim Mganga.
“Kassim aliambiwa atafute kampani ya kuja nayo huku ndipo akaona Aunt anafaa kwa kuwa mwenyewe amedai ni mtu wake wa karibu,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kwamba, baada ya wawili hao kufika nchini humo, walipanga katika hoteli moja kisha kuanza kujiachia kwenye viwanja tofautitofauti wakila bata ndani ya Jiji la New York.
Staa wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel Grayson.
Baada ya mwanahabari wetu kunasa mchapo huo, alimtafuta Aunt kupitia WhatsApp hakupatikana, bahati nzuri Kassim alipatikana na kusema:“Tumekuja kwa mwaliko wa ubalozi wetu, Aunt ni mshkaji wangu kwa hiyo usishangae sana nikila naye bata,” alijibu Kassim.