Rehema Chalamila amekasirika na kwa jinsi ambavyo anawachukia wauza unga, hana hata chembe ya huruma kwa Jackie Cliff aliyekamatwa na madawa ya kulevya huko Macau, China mwezi December mwaka jana, 2013. Awali Ray C aliweka picha Instagram ya Jackie akiwa amekamatwa na vyombo vya dola nchini humo bila kuandika chochote, lakini mizuka ya kufunguka ilikuja kupanda baada ya baadhi ya followers wake kumtetea Jackie. “Wewe tulia mi na hasira maana najua walichonifanya Hawa wauzaji!?!niliingia kwenye madawa na niliwapa kila Kitu hawa wauzaji ili nipate unga maana tayari nilikuwa nimeshaathirika,hawakunionea huruma pamoja na aibu yote walichotaka wao ni pesa ili nipone ndio niheme!!!!!!nilipokuwa na hela walinithamini ila nilipoishiwa walinilaza kwenye box na arosto!!!niliwaomba hata kidogo ili nisiumwe but hawakunielewa ingawa nilishawapa mamilioni ya hela Na nyumba nikauza!!!!!!!sikia tu arosto na omba isiwahi kutokea kwa ndugu yako wala mtoto wako!!!!!!jinsi mama yangu alivyohangaika Na Mimi k**aninA huyu jacky afe tu mbwa mkubwa!!!!na muuaji ndugu za watu wanalala barabarani mmpaka tunaimbwa teja wa mapenzi!!!!yani acha kabisa!!!wafe wanyongwe,mafirauni wenye dhambi kubwa mbele ya mungu!!!ktk jina la yesu!!!!Wanyongwe!!!!!!!Kill them,” aliandika Ray C.
Na Gladness Mallya STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ameibuka na kusema kuwa anahitaji mume anayemzidi umri kwa miaka kumi. Akizungumza hivi karibuni kwenye kituo kimoja maarufu cha runinga, Ray C alisema anahitaji mwanaume mtu mzima anayemzidi miaka kumi, anayejitambua na asiwe mwanamuziki kwani anaamini akiwa na mtu kama huyo uhusiano wao utakuwa mzuri kuliko ule wa awali uliokuwa wa machungu. “Ninamtaka mwanaume anayenizidi miaka kumi kwani kwa sasa nina miaka 31 japokuwa kwa sasa nafanya kazi kwanza ili nirudi kwenye levo yangu na nitakuwa juu zaidi ya zamani kwa sababu najitambua japokuwa nina hamu sana ya mtoto lakini yote namwachia Mungu. “Nashukuru sasa hivi niko vizuri nakumbuka meneja wangu wa kwanza alinikataza nisiwe na uhusiano na mwanamuziki lakini ndiyo hivyo nikajikuta niko na Lord Eyes ambaye alianza kunichanganyia cha Arusha (bangi) bila mimi kujua na kujikuta ninaharibikiwa lakini nimeshamsamehe na ninamuombea heri katika maisha yake,” alisema Ray C. Aidha, Ray C alisema anamshukuru Mungu kwa sababu hana mume wala mtoto kwa sababu kwa jinsi alivyokuwa mwanzo angejenga picha mbaya sana kwa mwanaye. “Wakati nilipokuwa na matatizo nilijifunza mengi kwamba hakuna rafiki wa kweli kwa sababu walinipenda nikiwa mzima lakini nilipokuwa naumwa hakuna hata mmoja aliyenipigia simu kunijulia hali zaidi ya mashabiki zangu tu kwa hiyo nimebadilisha mfumo wa maisha yangu,” alisema Ray C. Miezi kadhaa iliyopita, mwanamuziki huyo alitangaza kuachana na madawa ya kulevya ambayo alikiri kuwa yalimharibia mwenendo mzima wa maisha yake.
Rehema Chalamila aka Ray C haisahau kabisa tarehe 8/11/2013 kama siku ambayo aliachana rasmi na matumizi ya dawa za kulevya na kupewa tiba kwa msaada wa rais Jakaya Kikwete. Ray C aliitumia siku hiyo kuungana na watu walioacha kutumia dawa za kulevya, na kwa pamoja walijipongeza kwa hatua hiyo. Kupitia Instagram, juzi (November 8) Ray C alipost picha akiwa na watu hao na kuandika ujumbe kuonesha upendo wake kwao, na kwa kuona watu wanaweza kuacha kabisa matumizi ya dawa hizo anaamini Tanzania bila dawa za kulevya inawezekana. “@ Nawapenda sana hawa wenzangu wote tuligundua tatizo tukasaidiwa na sasa Tumepona na tunamshukuru Mungu....Tanzania bila Madawa ya Kulevya inawezekana.” Baada ya kumaliza kupeana pongezi na elimu zaidi kuhusu athari za matumizi ya madawa ya kulevya, Ray C aliielezea siku hiyo kupitia Instagram. “Looooong day but am very happy....8/11/2013 Will always remember ths special Day......God!I heart You....” aliandika Ray C
STAA wa Bongo Fleva Rehema Chalamila‘Ray C’ ameamua kuianika gari yake ambayo anatembelea kwa sasa ... Gari hilo ni aina ya Jaguar ambalo namba zake za usajili hazionekani vizuri ila mwishoni zinasomeka T…CHL,huku akiandika kwenye instragram kuwa… Jaguar don't care...CHL means Chalamila Family.....