Lungi Mwaulanga akiwa kwenye pozi.Msanii wa filamu, Lungi Mwaulanga ametoa kali baada ya kusema kuwa,
bila kuvaa nguo zinazoanika baadhi ya sehemu zake ‘muhimu’ hasikii raha.
”Najua kuna ambao wanakereka na uvaaji wangu lakini nadhani hawana sababu ya kukereka. Napenda kuvaa ninavyojisikia kwa hiyo hata nikivaaje, ni mimi na maisha yangu,” alisema Lungi.
ODAMA: NAANZAANZAJE KUMFICHA BWANA’NGU?
Stori: Rhoda joSIAH
Mwanadada anayeuza nyago kwenye filamu za Kibongo, Jennifer Kyaka ‘Odama’ amekanusha tuhuma ya kumficha mwandani wake na kufunguka kuwa, marafiki na familia yake wanamjua hivyo haoni sababu ya kumfanya kila mtu amjue.
Odama alikuwa akizungumzia madai ya kumficha mwanaume aliyezaa naye huku baadhi wakisema, hataki mtu yeyote amjue kwani ni mume wa mtu.
“Hivi naanzaanzaje kumficha mwandani wangu? Halafu nimfiche ili iweje? Ndugu na marafiki zangu wanamjua, wasiomjua wawe na subira, kila jambo lina wakati wake,” alisema Odama ambaye juzikati alinaswa akiwa ‘very close’ ukumbini na mwanaume aliyefahamika kwa jina la Daudi ambaye ni mume wa mtu.