MTANGAZAJI wa
Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kinachorushwa kupitia Radio Times,
Hadija Shaibu ‘Dida’ amefunguka kuwa kamwe hawezi kufanya kazi Ikulu
kutokana na vimini anavyovitinga.
Mtangazaji wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani wa Radio Times, Hadija Shaibu ‘Dida’.
Akizungumza
na Amani, Dida, alisema kuwa anafurahia sana kazi anayofanya kwa sababu
inamruhusu kuvaa nguo yoyote anayojisikia vikiwemo vimini.
“Kufanya kazi Ikulu ningeshindwa
kwani kuvaa nguo ni kwa sheria, huwezi kujivalia tu, kazi yangu nipo
huru naweza kuvaa kitu chochote kile nikajisikia nina amani, lakini
Ikulu lazima utinge koti na kuchomekea,” alisema Dida.