Akichonga na paparazi wetu, Bond alisema baada ya kulazishwa kwa muda mrefu na Aunty Lulu, kwa mara ya kwanza alijikuta amepima Ukimwi na bahati nzuri walikutwa wako salama.
“Kipindi nikiwa na uhusiano wa kimapenzi na Aunty, alinilazimisha mpaka tukaenda kupima Ukimwi tukajikuta tupo salama ndiyo tukaendelea na mapenzi yetu na tulikuwa na tabia ya kupima mara kwa mara lakini nawashangaa wanaosema nimeambukizwa ngoma,” alisema Bond