RAIA wa Nepali, Master Nau, aliyefanyiwa vipimo na kugundulika kuwa na urefu wa sentimita 40 aliposafiri kutoka katika kijiji chake kilichopo kusini- magharibi mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Kathmandu.
Mwanaume huyo, mwenye umri wa miaka 73, anayetembelea baiskeli anataka atambulike katika Rekodi za Dunia za Guinness 'Guinness World Records' kama mtu mfupi kuliko wote duniani katika kundi la watu wasioweza kutembea.
Akiongea na wakala wa shirika la habari la AFP baada ya kurudi kijijini kwao, Bhairahawa, Master Nau alisema ana furaha sana.
Mpwa wa Master Nau, Seema Sheikh, alisema : 'mjomba wake ni mzoefu wa kusafiri na anapenda kukutana na watu na kuzungumza kuhusu maisha.'
'Anapenda pia chakula cha moto na chenye ladha nzuri pamoja na kusikiliza nyimbo za Kihindi na Kinepali. Mara kwa mara tunakodi madereva wa kumpeleka sokoni maana anapenda kwenda huko pia.'
'Tatizo analokumbana nalo ni kwamba, popote anapokwenda, watu huacha shughuli zao na kuanza kumwangalia yeye. Umati ukusanyika mahali alipo jambo linalosababisha usumbufu.'
Mnepali mwingine aitwaye, Chandra Bahadur Dangi, 74, anashikilia rekodi ya dunia ya kuwa mtu mfupi kuliko wote katika kundi la watu wanaoweza kutembea akiwa na urefu wa sentimita 54.6
Maofisa kutoka Rekodi za Dunia za Guinness wameahidi kufuatilia madai ya Master Nau na ikionekana ana vigezo sahii atatangazwa.