Anaitwa Gabriel Munissi mkazi wa Mwanza ambae Polisi Ilala Dar es salaam ilithibitisha kwamba ndio amehusika kufanya mauaji ya watu wengine wawili kabla ya yeye kujiua huku ikiaminika ni kutokana na wivu wa kimapenzi.
Kama hukuipata hii taarifa ni kwamba Gabriel alikwenda Ilala na kusimama nje ya nyumba moja iliyokua na fensi na geiti jeusi kusubiria atoke Mwanamke anaetajwa kuwahi kuwa mpenzi wake na kisha baada ya Mwanamke huyo kutoka huku akiendeshwa na mwanaume mmoja kwenye Toyota Surf na kukiwa na abiria wengine wawili kwenye gari, Gabriel ndio alianza kufyetua risasi ovyo.







