Hivi wanawake ni watu wa aina gani? naombeni ushauri jamani, nilikuwa na mpenzi akanisaliti akaenda kuolewa na lijibaba nikatafuta mwingine,nimezaa nae mtoto mmoja natunaishi kwa furaha.cha ajabu ameanza kunitumia mesegi,mojawapo imeandikwa hivi nanukuu "Najua nilikukosea samahani sana ila naomba umuache huyo mwanamke, amin nitamlea mtoto wako kama wakwangu kumbuka unafahamika mpaka nyumbani familia yangu inanicheka kwa nilichokifanya".huyu mwanamke ninayeishi nae kaona hiyo massage kaniambia nimsamehee na yuko radhi kuondoka....Sasa nifanyaje nishaurini
By Silvester Limota







