“TANESCO KUONGEZA GHARAMA ZA UMEME KWA 68%, KAMA HUWEZI KULIPA TUMIA KIBATARI”….NAIBU WAZIRI WA NISHATI

 Naibu Waziri wa umeme, Mh George Simbachawene, amesema kwamba serikali imekubali TANESCO waongeze gharama za umeme kwa 68% kama walivyokuwa wameomba.
 

Simbachawene ameitoa  kauli hiyo wakati akiongea katika kipindi cha Kumepambazuka kupitia Radio One leo asubuhi. 


Amesema kwamba hata kama TANESCO wakiongeza gharama za umeme hadi kufikia Tsh 800 kwa unit bei hiyo ni nafuu kuliko gharama za kununua mafuta ya taa.
 
Mh Simbachawene ametahadharisha kwamba kama mtu ataona kwamba gharama za umeme ni kubwa, basi akawashe kibatari au akae gizani.
 
Source: Jamiiforum  via Kumepambazuka, Radio One.