NYOTA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa filamu yake aliyoitoa kumuenzi marehemu Steven Kanumba iitwayo After Death ilimlostisha kwa kuwa ilimpatia hasara kubwa.
Alisema hasara aliyoipata na ambayo hata wasanii wenzake huipata inatokana na uwepo wa wasambazaji wachache wa kazi za wasanii, kitu kinachowafanya watu hao kujipangia bei bila kujali gharama ambazo wameingia katika utengenezaji wake.
-GPL