Siku hizi watu wengi wamekuwa na mtindo wa kuajiri wasichana wa kazi ili kusaidia kazi za nyumbani....
Hatukatai, pengine mama mwenye nyumba anaweza kuwa anazidiwa na kazi,kama kufua nguo za mzee,watoto,kunyoosha, kuandaa chakula nakadhalika.
Lakini kuna wanawake wengine unakuta wako wawili tu, yeye na mumewe, eti nao wanaweka house girl sijui wa nini? Tena wengine sijui ni sifa eti anaajiri wawili kabisa .Kwa kazi zipi?na wewe ufanye kazi gani? Ya kupaka rangi kucha na kuchat kwenye mitandao? Halafu bila aibu unasifia chakula alichoandaa house girl mbele ya mumeo.
Na unaangalia tu house girl anamnawisha mikono mumeo na kumkausha na taulo,wewe upo tu kwenye kiti kama umegundishwa na super glue vile.
Huyo jamaa yako akila chakula kitamu cha house girl, si atataka ale na kile cha usiku aone utam wake? Hapo ndipo usaliti unapoanzia na ukizingatia mahouse girl walivyo na heshima...!!
Baba akifika na kamzigo anapokelewa kwa mikono miwili na anapigiwa goti, wakati huo we upo upo tu kama koti la mvua linalosubiri masika....Pole!!!
Sijui ndio kusema hamuelewi mko pale kwa ajiri gani? Mumeo akisifiwa kazini nguo zake zinang'aa atamkumbuka house girl, akisifiwa kwamba ananawili atamkumbuka house girl, akisifiwa kwamba viatu vyake vinang'aa atamkumbuka house girl
Mbona umeguna??? House girl si ndo anaye fanikisha hayo yote wakati wewe ukiwa bize ku upload picha facebook? Mwisho wa siku unatemwa kama big G iliyo chacha, halafu watu wanabaki kushangaa mbona jamaa kamuacha mwanamke mzuri vile halafu kabeba house girl?
Kumbe mwanamke yule ni janga la kitaifa hajui moja wala mbili .Badilikeni jamani ma house girl watawapiga bao.