Jengo la pili kwa urefu New York City linalojulikana kwa jina la Empire State Building likiwaka taa zenye rangi ya bendera ya South Africa. Unaweza kuelewa kuwa ni jinsi gani dunia kwa ujumla imeguswa na kifo cha kiongozi huyo aliekuwa mstari wa mbele katika mapambano ya ubaguzi wa rangi duniani.
Hapa ni makao makuu ya Umoja wa Mataifa Duniani New York City nako bendera inapepea nusu mlingoti kama unavyoona.
Apollo ni sehemu maarufu sana hapa New York City sehemu hii inapatika 125th Street Up town Harlem. Apollo ni maarufu sana kwani ndiyo chimbuko la masuper star wote wa Marekani bila kupitia hapa na kupata mzimu kwa kugusa mti maalum unaopatika ndani ya jengo hili basi uwezi kuwa super star. Kila jumatano kunakuwa na mashindani ya kumpata super star mpya kwa jina la (Amateur Night). Apollo wanatambua mchango wa Mandela na kama unavyoona jina lake lina shine juu ya ubao wao wa matangazo kama njia ya kumuenzi kiongozi huyo wa Africa.
Mishumaa inawaka na picha ya Mandela ikiwa juu na chini watu wakisign na kuweka michumaa pamoja na maua. Hapa ni Apollo karibu na mlango wakuingilia ndani ya jengo hili.