UFOO SARO APONA, SASA KUREJEA KAZINI

MWANDISHI wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufoo Saro ambaye hivi karibuni alikumbwa na madhila ya kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya na mzazi mwenzie, kwa sasa afya yake imeimarika na kurejea kazini.


Kamera ya Matukio iliweza kumkamata katika mmoja ya mkutano wa waandishi wa habari wakati akiuliza swali.

Mmoja ya wafanyakazi wenzake ambaye hakupenda kuwekwa wazi jina lake alisema, "Ufoo Saro yupo fiti na sasa ameshaanza tena mikikimikii ya kazi yake, japo kuna wakati akikaa peke yake anakuwa mpweke na mwenye mawazo sana," Kikubwa tunachokifanya sisi ni kutoongelea tena lile tatizo... Aliweka wazi mfanyakazi huyo.