USHIRIKINA NDIO SABABU YA KUVUNJIKA KWA NDOA YA THEA

SIKU chache baada ya ndoa ya mastaa wawili wa filamu Bongo, Salome Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ na Michael Sangu ‘Mike’ kuvunjika, imedaiwa mambo ya kishirikina yanahusika kwani mauzauza yalianza siku nyingi zilizopita.

Thea na Mike siku ya ndoa yao.
Mtu wa karibu wa mastaa hao aliyeomba jina lake liwekwe kapuni alidai kuwa mara kadhaa wasanii hao wamekuwa wakikumbwa na mambo ya ajabu yaliyoashiria kuwa ndoa yao haina uhai.
“Unajua kwa nyakati tofauti pete za ndoa za Thea na Mike ziliwahi kuwatoka kiajabu vidoleni wakiwa chooni. Haikuwa jambo la kawaida na wenyewe walishituka na kukosa amani,” alisema mtoa habari huyo.
Hata hivyo, wahusika wamekuwa wakiamini kuvunjika kwa ndoa yao ni mipango ya Mungu licha ya Mike kuhisi kuwepo kwa nguvu za giza katika kuachana kwao.
“Mimi naamini kila linalotokea ni mipango ya Mungu lakini katika hili mmh, napata mashaka,” alisema Mike.
Naye The alisema: Mungu hakupanga tu tuendelee kuwa kwenye ndoa, kwa hiyo limetokea na maisha yanaendelea.”