Yapo madai kwamba, Mchungaji Christopher
ambaye ni msaidizi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God ‘TAG’,
Kinondoni jijini Dar amekuwa akikerwa na tabia chafu anazozisikia za
msanii Lulu Mathias Semagongo ‘Antu Lulu’.
Lulu alisema: “Jamani, kama ni kubadilika
najitahidi. Hata Mchungaji Christopher wa TAG, Kinondoni kwa Mchungaji
Swai amekuwa akiniambia nirudi kanisani akaniombee.
Unajua yule ndiye aliyenilea kiroho nikiwa nasoma Sunday School pale,
sasa anaposoma habari zangu anaumia, lakini sasa nimebadilika sana.”






