Wanakwaya wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God, Hanipher na Godfrey (mtoto wa mchungaji) walionaswa wakiwa kichakani.
Hivi karibuni mjini Iringa, wanakwaya wawili wa Kanisa la Tanzania
Assemblies of God, mwanamke alijitambulisha kwa jina moja la Hanipher na
mwanaume aliyesema anaitwa Godfrey, walinaswa usiku kichakani katika
mazingira yaliyojaa utata, Risasi Jumamosi linakupa kisa kamili. NI MAKABURINI Tukio hilo la kushangaza, lilijiri
kwenye eneo la Makanyagio ambalo lina makaburi ya awali katika Manispaa
ya Iringa licha ya kuwepo na nyumba za wenyeji pia. KAZI YA SUNGUSUNGU Kwa mujibu wa chanzo chetu,
wanakwaya hao walinaswa na sungusungu ambao siku za hivi karibuni
wamekuwa wakifanya ‘patroo’ katika eneo hilo na la Isoka kufuatia kuwepo
kwa matukio ya wakazi wake kuvamiwa, kupigwa na kuporwa mali. SIKU YA TUKIO Siku ya tukio, sungusungu hao
wakiwa katika majukumu yao waliwaona wanakwaya hao wakiacha njia kuu
na kuchepukia porini umbali unaokadiriwa kuwa mita 20 kutoka barabarani. “Ilibidi sungusungu wawafuate hadi kule kichakani, ndipo walipowakuta
katika mazingira tata na yenye maswali mengi bila majibu. Mbaya zaidi,
yule mwanamke alikuwa na mtoto wa mwaka mmoja mgongoni,” kilisema chanzo
chetu.
Wanakwaya wakifunguka kueleza kisa cha kuwa kichakani usiku mnene.
WAPEWA KICHAPO, WAJIANIKA Chanzo kikadai kuwa,
sungusungu hao waliwapa kichapo chepesi ili waweze kusema walikuwa
wakifanya nini na wao ni akina nani, ndipo mwanamke huyo akaweka wazi
mambo kwamba, yeye ni mkazi wa Kitongoji cha Isoka ilhali kijana huyo ni
mwimbaji mwenzake wa kwaya lakini pia ni mtoto wa mchungaji wa kanisa
hilo. ETI? Katika hali ya kushangaza, mtoto huyo wa
mchungaji huku akiomba samahani kwa kunaswa kichakani, alisema eti
kilichowapeleka huko muda huo wa usiku ni kumsaidia mwanamke huyo
kumwingizia nyimbo za dini kwenye simu yake!! AKIRI SI MWENENDO MWEMA Pamoja na yote, Godfrey
alikiri kuwa kitendo cha kuingia kichakani na mwanamke muda huo wa saa
2.15 usiku kilikuwa ni hatari kwao kiimani na hata usalama wa miili yao
kwa ujumla. Kiimani alikuwa na maana kwamba, kuonekana kichakani watu waliookoka
hakutoi picha nzuri kwa jamii inayotakiwa kuhubiriwa ili watu wamrudie
Mungu, usalama wa miili ni kama vile kuumwa na nyoka au wadudu wengine
wenye kudhuru. SUNGUSUNGU NAYE Akizungumza na Risasi Jumamosi,
mmoja wa sungusungu hao alisema haikuwa rahisi kwao kuamini kwamba
wawili hao waliingia kichakani kuingiziana nyimbo kwenye simu. “Hivi kweli mtoke barabarani muingie kichakani kisa kuwekeana nyimbo
kwenye simu, inaingia akilini kweli? Labda bwana,” alisema sungusungu
huyo bila kutaja jina lake akidai wana bosi wao ndiye alitakiwa kusema.
Baada ya kuwatembezea kichapo na wawili hao kuomba msamaha, sungusunga
hao waliachia na kuwaonya wasirudie tena kukutwa vichakani usiku.
Kuna kitu ningependa niwashirikisha marafiki wa ukurasa huu ingawa ni aibu lakini ni vyema pia na akina dada wenzangu na hata vijana wa kiume wajifunze kutoka kwangu.
Mimi ni binti wa miaka 30 na nimebahatika kupata watoto wawili wakiume na wakike na namshukuru muumba kwani wana afya tele.
Niliolewa miaka 5 iliyopita na kijana mmoja ambaye tulikuwa wapenzi kwa takribani miaka sita na baadae tukaona ni vyema tuoane.
Katika maisha yetu ni kweli baba watoto amekuwa mtu asiye na makuu na mwenye kujali na mara nyingi tumekuwa hatuna matatizo madogo madogo kwani yeye ni mzee wa mesheni town.
Nianza kusikia mtaani kuwa mme wangu sio riziki lakini nilipuuzia kwani siku hizi kijana akiwa na maendeleo kidogo na ni handsome basi watu hawataacha kumpa kashfa kibao na hasa ukizingatia kazi za mishemishe nazo huwa na majanga yake.
Hata nilipoambiwa kuwa kwa nini anakuwa karibu sana na waarabu nilipuuza kwani mimi nilimwamini sana mme wangu. Na pia nilijiuliza mbona deal zake nyingi ni dubai na oman kwa hiyo ni kawaida tu ukizingatia huko ndio kuna watu wa rangi hiyo.
Kuna wakati nakumbuka niliwahi kumuomba ruhusa niende kijijini kwetu nikawasalimie wazazi na bila hiyana akaniwekea gari tayari pamoja na vijisenti vya kuwapa wazazi na kuwa ningekaa kule kwa muda wa wiki mbili.
Kwa bahati mbaya sikuweza kukaa siku zote kwani kuna tatizo lilijitokeza ikanibidi nirudi mapema bila kumwambia nikijua tungejadiliana kunako nyumbani nikifika
Sikuamini kwani kufika nyumbani tena kwenye chumba.chetu cha kulala nikaona boxer ngeni nikamuuliza hii ni ya nani? Nakumbuka akanijibu kuwa ni ya shamba boy, nikajaribu kuuliza ilifikaje ndani kwetu akadai usiku alikuwa anaogopa hivyo akawa akilala na shamba boy.
Ulikuwa ni mtihani kwangu ingawa ilinibidi niamini huku nikijiuliza kama baba anakuwa muoga sie wana famialia tunaohitaji ulinzi wake itakuwa vipi? Basi yakaisha na maisha yakaendelea.
Ilipita miezi na sasa ni miaka ambapo wiki iliyopita nimemfumania live akiwa na jibaba la kiarabu tena bila aibu juu ya kitanda chetu cha ndoa.
Nilishtuka na kidogo nizirai lakini nilijikaza hasa ukizingatia sikutaka majirani wapate hili, kwa aibu akanifuata na kuniambia nimsamehe kwani ni mara ya kwanza na amefanya hivyo ili apate deal la kwenda Dubai kufanya shoping ya nyumba na ofisi yetu mpya.
Kweli niliamua kumuachia nyumba na nimeondoka na wanangu mpaka sasa nipo nimepanga sehemu ambapo nimeanza maisha mapya na kamwe hata niona maana ni laana.
Mkazi wa Mtaa wa Lagos, Wazo Mivumoni, Msitu wa Pande jijini Dar es Salaam, Nuru Makala ‘Baba Eliza’ (42) Jumatano iliyopita alikumbwa na majanga baada ya mwanaume aliyejulikana kwa jina la Yusuf Ally ‘Mgosi wa Ndima’ kudai amemfumania Baba Eliza akiwa na mkewe ambaye jina halikupatikana.
Tafrani hiyo ilijiri usiku wa Jumatano iliyopita, Juni 18, mwaka huu kwenye nyumba yake iliyopo Mtaa wa Lagos, Msitu wa Pande.
Akizungumzia tukio hilo mbele ya wanahabari waliokuwa eneo hilo wakisaka habari, Yusuf Ally ambaye ni mume wa mwanamke aliyefumaniwa alisema:
“Nilikuwa katika harakati za kumchunguza mke wangu kinyemela kwa siku nyingi kama anachepuka, nikabaini kuna mawasiliano yenye shaka kati yake na huyo jirani yangu.
“Nilipomuuliza mke wangu alikiri, akasema amekuwa akimwambia jirani yangu kwamba haiwezekani lakini jamaa anakomaa tu anamwambia wakutane, tena wakutane humu ndani.
“Ndipo nilipoamua kumuandaa mke wangu kwa mtego amwambie jamaa kuwa leo (siku ya tukio) sitakuwepo na sitarudi ili kumpa nafasi jamaa kuja kujinafasi. Baada ya kukamilisha mtego niliwasiliana na kamanda wa sungusungu wa eneo hilo, Kapteni Makumba na kumuelezea kinagaubaga.
“Kapteni Makumba aliwaandaa vijana wake ambapo kuanzia mishale ya saa mbili usiku walijibanza kwenye kichaka kilichopo mbele ya nyumba huku akifanya mawasiliano na mimi.”
Mgoni akiomba Msamaha.
Yusuf aliendelea kudai kuwa, ilipotimu saa tano usiku kukiwa kumetulia, Baba Eliza alionekana akikaribia nyumba ya jirani yake huyo kwa hatua za kunyata na kuangalia kulia na kushoto kisha akazama ndani huku mkononi akiwa ameshika kifurushi kilichobainika baadaye kwamba kilikuwa na machungwa kadhaa.
Alisema muda mfupi baada ya kuingia, sungusungu mmoja alikwenda kujibanza kwenye dirisha la chumba na kupiga chabo kilichokuwa kikiendelea ambapo alimshuhudia Baba Eliza akichojoa nguo chapchapu tayari kwa mtanange, sungusungu huyo akawatonya wenzake.
Yusuf akazidi kusema kwamba wote walitoka kichakani na kwenda kuvamia chumbani ambapo walimkuta mkewe aliyekuwa bado hajaanza kuvua nguo kwa sababu alijua majanga yatatokea muda si mrefu akiwa anajiandaa kufanya hivyo kiaina.
Baada ya hali kuwa shwari, Kamanda wa Sungusungu, Kapteni Makumba alianza kumsomea mashitaka jirani huyo aliyekuwa mtupu muda huo mbaye hakuwa na la kusema zaidi ya kuomba radhi na kumtupia lawama ibilisi kwamba ndiye aliyemshawishi na haikuwa amri yake.
Raia aliyeshuhudia mkasa huo akionesha sehemu ya kitanda iliyochafuliwa na mgoni kwa kinyesi.
Sungusungu walimtaka Baba Eliza kumlipa fidia ya shilingi milioni moja mwenye mke kwa kitendo cha kumdhalilishia ndoa yake.