FAHAMU JINSI UGONJWA WA KISUKARI UNAVYOSABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA UGONJWA WA FIGO

 
Watu wenye kisukari, wanashauriwa kufanya uchunguzi wa figo zao mara moja kwa mwaka ambapo utachunguzwa kama una dalili zozote zinazoashiria matatizo ya figo. Utapimwa mkojo kwa ajili ya kuchunguza kiwango cha protini iitwayo Albumin au Microalbuminuria.
Kabla ya kuanza kueleza matibabu ya matatizo haya nikumbushe kwa kusema kuwa kuwepo kwa kiasi kingi cha protini katika mkojo ni mojawapo ya dalili za kuwepo kwa tatizo katika figo.
Mgonjwa wa maradhi haya ni lazima katika vipimo atakavyofanya daktari aangalie  kiasi cha Urea Nitrogen katika damu (BUN), kiwango cha Creatine katika damu (serum creatinine) na kiasi cha protini katika mkojo wa saa 24 (24-hour urine protein).

Kabla ya kufafanua tiba ni muhimu kukumbusha pia kuwa ni vyema mgonjwa akaangaliwa kiasi cha madini ya Phosphorus, Calcium, Bicarbonate, PTH, na Potassium katika damu.
Itakuwa vema kama daktari ataangalia kiasi cha wingi wa damu (Haemoglobin), na wakati fulani kufanya Biopsy ya figo kwa ajili ya uthibitisho wa tatizo.

Matibabu
Matibabu ya ugonjwa wa figo unaotokana na kisukari ni muhimu sana kufanyika haraka baada ya dalili kujitokeza. Lengo kuu la matibabu ni kufanya figo zisiendelee kuathirika. Mojawapo ya njia bora kabisa za kusaidia hilo ni kudhibiti kiwango cha shinikizo la damu kuwa chini ya 130/80 mmHg.

Zipo dawa ambazo husaidia tatizo hili kama vile zile za jamii ya Angiotensin Converting Enzyme Inhibitors kwa mfano Captopril pamoja na zile za Angiotensin Receptor Blockers zimeonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kushusha shinikizo la damu wakati huohuo kudhibiti kasi ya kuharibika kwa figo kutokana na kisukari.
USHAURI
Wagonjwa wanashauriwa kula lishe yenye kiwango kidogo cha mafuta, matumizi ya dawa za kudhibiti kiasi cha mafuta mwilini, na kufanya mazoezi mara kwa mara kama vile kutembea kwa saa mbili na wawe wanakunywa maji kwa wingi kabla na baada ya matembezi kwani husaidia sana kuzuia au kupunguza kasi ya kuathirika kwa figo.

Wagonjwa wanashauriwa kubadilisha aina ya chakula wanachokula, kutumia dawa za kisukari kama inavyoshauriwa na daktari na kuchunguza kiwango  cha sukari kila mara kwani husaidia kuzuia tatizo hili.
Waliopatwa na ugonjwa wa kisukari wanaweza kuwa na chombo cha kujipima wenyewe kiwango cha sukari mwilini mwao, ugonjwa huu huchangia sana kuua nguvu za kiume.