Showing posts with label AFYA. Show all posts
Showing posts with label AFYA. Show all posts

MAHUSIANO: MAPENZI KIPINDI CHA UJAUZITO

Leo naomba kuleta maada hii mezani baada ya mabishano mengi na maswali mengi kutika kwa wadau wangu Nimefikia hatua mara baada ya
mabishano na mijadala kadhaa ya watu wazima kuhusu mapenzi, staili na madhara kipindi cha ujauzito! kwa leo mimi ntasema machache nnaimani mengi yanajulikana tayari.
                  Kabla yote ieleweke kwamba wapo baadhi ya wanawake ambao inapofika kipindi cha Ujauzito huwa hawapendi hata kuguswa bega na waume zao, kama hali ikiwa hivi, mume usimmaind sana, elewa ni mapito tu na "atarudi kundini soon" Pia wapo baadhi ya wanawake ambao wanapokuwa na ujauzito basi hamu ya kufanya mapenzi huongezeka maradufu na inawezekana wakataka "Uroda" Kila siku, hapo pia mzee mwezangu jua ni mapito, yataisha tuu! Kikubwa ni kuelewa Mkeo yupo katika hali gani na kujitahidi kadri ya uwezo wako kwenda nayo sawa.
            
Mbali na hayo napenda niseme kuwa "INAWEZAEKANA" kabisa Mume na Mke Kufanya mapenzi kipindi cha Ujauzito wa Mke mpaka siku anayojifungua, bila kuhofia eti utamjeruhi mtoto maana kabla haujafikia alipo mtoto kuna Matabaka ambayo yanamkinga mtoto na uvamizi wa nje hasa wa "Dudu" ya Baba!
Kuhusu Staili nakuomba mume usiwe unampinda sana Mkeo maana utakuwa unamuumiza tumbo, piga zile za kale tu! Pia Kama Mke unawasiwasi na Hali yako ni vizuri ukamwona Daktari wako wa Kliniki kwa maelezo au vipimo vya ziada!

VIDONDA VYA TUMBO VINAVYOWATESA WENGI BILA KUJUA! SOMA HAPA KUJIJUA


Vidonda vya tumbo ni ugonjwa unaowasumbua watu wengi,  wanaume na wanawake na hata watoto wadogo. Tatizo hili husumbua sana na kumfanya mgonjwa asiweze kumudu shughuli zake za kila siku.
Ugonjwa huu huathiri kwa ujumla katika suala zima la afya.
Tatizo hili huanza taratibu na dalili za awali huwa hazionyeshi kama mtu ana ugonjwa huu.

Chanzo cha ugonjwa
Ugonjwa huu hutokana zaidi na maambukizi ya bakteria waitwao ‘Herictobacter Pylori’ au maarufu kama H. Pylori  hushambulia tabaka la ndani la tumbo.

Aina hii ya bakteria ni wagumu kufa kwa kuwa wana uwezo wa kuishi kwenye  mazingira ya tindikali tumboni. Tumboni kuna tindikali ya Hydrochloric Acid ambayo husaidia katika mmeng’enyo wa chakula.
Bakteria hawa wanaposhambulia tabaka la ndani la kizazi, hutegemea vishimo vishimo ambavyo ni vidonda hivyo tindikali inapotoka huchoma kwenye hivyo vidonda na kumfanya mgonjwa ahisi maumivu makali.

Aina za vidonda vya tumbo
Vidonda vya tumbo vipo vya aina mbili, kwanza ni vile vilivyopo mwanzoni mwa tumbo la chakula, Gastric Ulcers na ya pili ni Duodenal Ulcers katika sehemu ya pili ya tumbo. Maumivu na dalili za aina hizi mbili hufanana sana.

Ili kutofautisha aina hizi za vidonda, vipimo maalum hufanyika kama vile ‘OGD” na “Barium Meal’, vipimo ambavyo hufanyika katika hospitali za rufaa.
Dalili za ugonjwa
Hapa tutazungumzia dalili kuu za vidonda vya tumbo kwa ujumla. Mgonjwa wa vidonda vya tumbo katika hatua za awali huwa hajigundui kama ana tatizo.

Mgonjwa hulalamika kuhisi homa za mara kwa mara na kujihisi kama ana malaria au homa ya tumbo ‘Taifoidi’, wengine hulalamika kutumia sana dawa za taifoidi lakini hakuna nafuu.
Mwili unanyong’onyea, maumivu ya viungo, kuhisi baridi kuumwa kichwa na tumbo kujaa gesi.
Mgonjwa pia hulalamika maumivu ya tumbo eneo la chembe ya moyo ambapo ni chini ya kifua na juu ya kitovu.

Maumivu ya muda mrefu husambaa tumbo lote na tumbo huunguruma mara kwa mara .
Maumivu ya chembe ya moyo yaani chini ya kifua na juu ya kitovu husambaa hadi kifuani na kuzunguka mpaka mgongoni.

Mgonjwa hulalamika kuhisi moto kifuani na maumivu yaani kiungulia. Akilala usiku hali ya moto huongezeka na mgonjwa akicheua hutoa majimaji ya moto na machungu.
Mgonjwa hupata choo kigumu na vipande vipande kama cha mbuzi na wakati mwingine huwa cheusi.
Mgonjwa hupoteza hamu ya kula na wakati mwingine hutapika damu. Macho hupoteza nguvu ya kuona kwa kuwa muda wote anakuwa na maumivu, mwili unachoka na anakosa raha kutokana na kuwaza sana juu ya maumivu anayopata kiasi cha kumfanya mgonjwa akonde.

Mkojo unakuwa wa njano sana, hufunga kupata choo kikubwa na kusababisha maumivu ya kiuno kwa ndani ambayo husambaa hadi miguuni. Hamu ya tendo la ndoa pia hupotea.
Uchunguzi wa ugonjwa
Uchunguzi wa awali hufanyika katika vituo vya afya na hospitali za wilaya, mikoa na rufaa. Ni ugonjwa unaotibika hospitali na  vipimo ni kama Ultrasound, OGD, Barium Meal na vipimo vya damu ili kuangalia maambukizi ya H. Pylori na wingi wa damu.

Choo kikubwa pia kitapimwa. Ni muhimu pia kuangalia matatizo mengine kwa undani. Kipimo cha OGD ambacho kitapitishwa katika mfumo wa chakula kitasaidia kutoa majimaji yatakayopimwa maabara.
Ushauri
Ni vema mgonjwa azingatie kuhudhuria hospitali kwani ugonjwa wa vidonda vya tumbo huchunguzwa na kutibiwa hospitali ingawa tiba huchukua muda mrefu.

Ugonjwa huu dalili zake zinafanana sana na saratani au kansa ya tumbo hivyo ni vizuri uwahi hospitali ili ugundulike mapema.Unaweza ukawa unatumia dawa nyingine pasipo uchunguzi wa kidaktari mwishowe ukajikuta tayari hali inakuwa mbaya na kusababisha utumbo kutoboka au kansa.

WATUMIAJI WA KUCHA BANDIA HEBU ONA KILICHOMTOKEA HUYU DADA


Msichana Sarah Greenaway mwenye umri wa miaka 17 amekosa kidole chake baada ya kutumia gundi ya kugandishia kucha bandia. Kidole cha dada huyo kilianza kubadilika kuwa bluu na baadae njano muda fulani baada ya kuweka gundi hiyo. Alikimbizwa hospitali na kufanyiwa upasuaji ambao ulimghalimu kidole chake huko kusini mwa Wales, Uingereza. Jamani uangalifu kwenye utumizi wa vipodozi muhimu.

TATIZO LA KUHARIBIKA MIMBA MARA KWA MARA, LIJUE HAPA

Tatizo la kuharibika mimba mara kwa mara kitaalamu huitwa ‘Recurrent pregnancy loss’. Mwanamke hujitahidi kutafuta ujauzito lakini inakuwa ngumu ujauzito kukua hadi kufikia kujifungua.
Hali hii huleta athari kubwa kwa mwanamke pamoja na kuathirika kiafya kutokana na mimba kuharibika mara kwa mara lakini pia huathirika kisaikolojia kwa kutopata watoto. Ni mojawapo ya tatizo linalochangia ugumba katika jamii.

Kipindi cha ujauzito huchukua majuma arobaini kuanzia mimba inapotungwa hadi mama anakuja kujifungua mtoto kamili.  Mtoto kamili na mwenye afya njema huzaliwa katika uzito wa kilo kuanzia mbili na nusu. 
Chini ya uzito huu ni watoto wenye matatizo na wanakuwa katika uangalizi maalumu hospitali chini ya usimamizi wa madaktari wa watoto.Kipindi cha ujauzito pia kimegawanyika katika vipindi vitatu ambavyo kitaalamu huitwa ‘Trimesters’, vipindi hivi ni vya miezi mitatu mitatu.  Miezi mitatu ya kwanza tunaita kipindi cha uumbaji. 
Katika kipindi hiki ndipo viungo vya mtoto vinapoumbwa na kukamilika.Mimba inayoumbwa ikiwa na kasoro mwili wa mama unaofanya kazi vizuri huitoa wenyewe, hapa ndipo tunapopata historia ya mama kwamba amepoteza mimba kadhaa zikiwa na umri wa chini ya miezi mitatu. Ni mara chache vyanzo vyake kutibika.
Vipo vyanzo vingi vinavyosababisha mimba changa ziwe zinatoka, vyanzo hivi ni rahisi kugundulika baada ya kuhudhuria hospitali kwa daktari bingwa wa magonjwa ya kinamama na uzazi.
Ujauzito kuharibika katika miezi mitatu ya kwanza chanzo ni mimba yenyewe.

Ujauzito kuharibika katika miezi mitatu ya pili hutokana na tatizo katika mlango wa kizazi wa mama kushindwa kushikilia mimba. Tatizo hili kitaalamu huitwa ‘cervical incompetence’.
Mama anakuwa na historia ya mimba kumtoka kuanzia umri wa zaidi ya miezi mitatu hadi sita.  Mimba inaendelea vizuri kwa zaidi ya miezi mitatu ya kwanza na inapofikia miezi mitatu ya pili inatishia kutoka hadi inatoka.

Vyanzo vya mlango wa kizazi kulegea vipo vingi navyo pia vinahitaji uchunguzi wa kina kwa daktari wa kinamama na ikithibitika hivyo, basi mlango wa kizazi utashonwa na mama atapata mapumziko ya muda mrefu na akija kujifungua atafunguliwa kwanza nyuzi kisha atajifungua.
Katika kipindi hiki hata mtoto anaweza kufia tumboni na chanzo kikuu kinaweza kuwa upungufu mkubwa wa damu kwa mama mjamzito, shinikizo la damu kuwa juu na sababu nyingine ambazo daktari atazigundua.

Kwa kawaida presha ya mama mjamzito inatakiwa isizidi 120 kwa 80.  Ikizidi hapo ni vema ufuatilie kwa daktari wako.
Shinikizo la damu kuwa juu kwa mama mjamzito dalili zake ni kuvimba miguu, kukosa pumzi wakati wa kutembea, maumivu ya kifua na wakati mwingine macho hayaoni vizuri, akipimwa mkojo ataambiwa kuna protini nyingi kwenye mkojo.
Presha ikizidi kupanda, basi mama mjamzito atapata kifafa cha mimba. Pamoja na dalili hizo, ataanza kurusharusha mikono na miguu na kuwa kama mtoto mwenye degedege au mgonjwa wa kifafa.
Ni dalili ya hatari kwa uhai wa mama na mtoto.

NINI CHA KUFANYA?
Matatizo ya kuharibika kwa mimba mara kwa mara au watoto kufia tumboni ni tatizo linaloathiri afya ya mama na jamii yake kwa ujumla kwa kila kitu.Kama nilivyoelezea hapo awali, tatizo hili lina ufumbuzi endapo mama atahudhuria hospitali mapema. Uchunguzi na tiba hupatikana katika hospitali za wilaya na mikoa popote nchini.

Muone daktari bingwa wa magonjwa ya kinamama na matatizo ya uzazi katika hospitali hizo. Epuka imani potofu katika masuala haya, fuatilia uchauri wa kidaktari.

APEWA TUZO YA HESHIMA KWA KUMPELEKA MKEWE AMBAYE NI MJAMZITO KLINIKI


Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal (kushoto) akimpa Elia Mwumbui tuzo ya heshima ya kuchangia kupunguza vifo vya mama wajawazito. Picha na Fedelis Felix 

Kwa desturi iliyojengeka nchini, wanaume wengi hawana utamaduni wa kuwasindikiza wake zao kwenda kliniki kupima ujauzito au kupeleka watoto.
Hali hii inatokana na mfumo dume uliojengeka au wanaume kuona aibu kufanya hivyo au kuhofia kuchekwa na wenzake.
Licha ya tatizo hilo kwa walio wengi, hali ni tofauti kwa Elia Mwumbui (26), yeye ni mmoja wa wanaume wanaofaa kuigwa kutokana na kuthamini akitekeleza kwa vitendo  uzazi wa mpango kwa kuhudhuria kliniki, akiambatana na mkewe.
Kwa kutekeleza hilo na kutambua mchango wake, Taasisi ya Madaktari Wahitimu wa Vyuo Vikuu vya Tanzania (TPHI), imemtunukia Mwumbui, Tuzo ya Heshima ya Kutambua Mchango wake, kwa kupunguza vifo vya wajawazito.


TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
“Sikujua kama ni raha kumsindikiza mke wangu kliniki, nimejifunza mengi ambayo kila mwanaume anatakiwa kumfanyia mke wake,” anasema Mwumbui
Mwumbui ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Matongo, Wilaya ya  Ikungi, mkoani Singida, aliwavutia watu wengi kutokana na mazingira anayoishi kijijini, kuamua kujitoa kwenda na mke wake kliniki, jambo ambalo ni nadra kuliona.
Dk Telesephory Kyaruzi, Mkurugenzi Mkuu wa THPI, anasema kuwa wameamua kutambua mchango wa Mwumbui katika kupunguza vifo vya wajawazito kutokana na wakati wote kuhudhuria kliniki pamoja na mke wake.
Dk Kyaruzi ambaye alimtunuku Mwumbui tuzo hiyo anasema  kuwa, ili mwanamke aweze kulea ujauzito na kujifungua salama, mwanaume ana mchango mkubwa, wenye kumhamasisha mwanamke hasa anapomwona  akimhudumia kwa vitendo kwani hujisikia vyema.
Tuzo hizo za heshima kwa kuwa mstari wa mbele kuboresha afya ya mama na mtoto nchini, zilizotolewa na THPI ziwatambua watu wanane.
Watu hao walitunukiwa tuzo hizo na Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal mapema Novemba mwaka jana, lakini kivutio zaidi alikuwa Mwumbui.
Mara baada ya kuitwa kuchukua tuzo hiyo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Mwumbui alishangiliwa na umati wa watu ulihudhuria, huku baadhi wakiimba “Shemeji, ...shemeji, ...shemeji,’ kitendo kilichomfurahisha kila aliyekuwapo eneo hilo.CHANZO MWANAINCHI

PETER MSIGWA AMBAYE NI MBUNGE WA CHADEMA AUGUA GHAFLA NA KUKIMBIZWA HOSPITAL

Mbunge wa Iringa Mjini Kwa Tiketi ya CHADEMA Mh.Peter Msigwa(Mchungaji) amezidiwa ghafla na homa na kukimbizwa hospital,hali hiyo imetokea wkt wakiwa kwenye shughuli za kichama.
madaktari wanamuhudumia vizurr na anaendelea vyema sasa.
Taarifa zaidi zitakujia,

KIJANA WA MIAKA 19 ANAUMWA NA UGONJWA WA AJABU KWA MIAKA 8 NA MADAKTARI HAWAONI TATIZO

KIJANA Haruni Kayombo (19), mkazi wa Mbalizi, Mbeya anaishi kwa mateso makubwa tangu mwaka 2006, baada kushikwa na ugonjwa wa ajabu uliomuanza ghafla.
Haruni Kayombo.
Katika mahojiano na gazeti hili akiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam, Kayombo alisema bado hajui hatima ya maisha yake kutokana na mateso anayoyapata usiku na mchana huku akitoa simulizi ya majonzi namna gonjwa hilo lilivyomtokea.
Alisema awali akiwa na umri wa miaka 11 alilazwa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya lakini baadaye wazazi wake walifariki dunia na hakupata kuwajua ndugu zake jambo ambalo anaona hakuna haja ya kuwa binadamu huku akionekana mwenye mateso makubwa.
“Sioni faida ya kuwa binadamu, niliugua kama utani, ilifika wakati nikajua kitu cha kawaida, nilishangaa kuona linazidi kuongezeka nilijua utakuwa ugonjwa wa muda mfupi,  lakini nikashangaa usiku na mchana mateso yanazidi.
“Ni tatizo ambalo hata mimi mwenyewe sijui chanzo chake, lilianza kama kauvimbe ka kawaida, sikutambua mapema na sikuwa na hela kwenda kwenye kituo cha afya kwa matibabu zaidi.
“Nilijipa moyo kuwa ipo siku nitakuwa sawa lakini kwa mpaka sasa nimeshakata tamaa, sina baba wala mama, hapa kweli kuna haja ya mimi kuitwa binadamu? Sina kazi na sikubahatika kusoma ni nani atakayeokoa maisha yangu?
“Maisha haya ni Mungu tu anayeweza kuniokoa, inaniuma sana! Ningekuwa na ndugu wangeweza kunisaidia japo hata pesa ya matumizi. Eee... Mola okoa maisha yangu (analia). Napenda kuishi kama binadamu wengine lakini kwa hali hii sina amani kabisa.
“Zamani wakati tatizo linaanza nilikuwa na tabia ya kusali mara kwa mara lakini nimefika hatua ya kukata tamaa na kuona hakuna haja.
“Namuomba rais aje anitembelee ajionee mateso ninayoyapata usiku na mchana, nimepangiwa kwenda kufanyiwa operesheni India lakini sijui lini na itakuwaje!” alisimua Kayombo na kumaliza na kilio tena.

Kama utakuwa umeguswa na tatizo la Haruni Kayombo basi usisite kutoa mchango wako kwenye namba yake ya simu, mtumie kwa njia ya M-PESA ama wasiliana naye moja kwa moja akiwa ndani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa namba +255764548607.

WANAFUNZI WA CHUO CHA UDAKTARI MUHIMBILI HATARINI KUPATA MAONJWA YA MLIPUKO NA YAKUAMBUKIZWA, SOMA KUJUA ZAIDI

AMA KWELI MGANGA HAJIGANGI
WANAFUNZI wanaosomea udaktari katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas) wanaishi katika mazingira hatarishi kwani wanaweza kupata magonjwa ya mlipuko na yale ya kuambukizwa wakati wowote.

Uchunguzi uliofanywa na Operesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers ndani ya majengo ya chuo hicho yaliyo karibu na taasisi ya mifupa (MOI), umegundua kwamba kwa miezi mingi, vyoo vinavyotumiwa na wanafunzi hao vimejaa na kuziba kabisa, hali inayowafanya vijana hao, licha ya kushindwa kupata huduma hiyo muhimu ya kibinadamu, pia kuwa katika hatari ya kupatwa na magonjwa ya mlipuko.

“Hali ni mbaya sana hapa kwa kweli. Hatuna huduma ya choo kwa miezi miwili hadi mitatu sasa, tunapobanwa na haja, hasa kubwa, hulazimika kukimbilia Kariakoo kwenye vyoo vya kulipia, hapa hapafai,” mmoja wa wanachuo hao aliiambia OFM na kuomba hifadhi ya jina lake.

Wanafunzi hao ambao walitoa ushirikiano wa kutosha kwa makachero wetu, pia walisema majengo mengi yanayotumiwa kama mabweni yao ya kulala, yamechakaa na hivyo kuwafanya wawe na hofu kubwa, kwani yanaweza kuanguka wakati wowote.

OFM ilishuhudia ngazi za kushuka na kupanda, zinazozunguka nje ya majengo hayo zikiwa zimechakaa vibaya huku vyuma vilivyowekwa pembeni kwa ajili ya kujishikilia vikiwa vimemongonyoka. Ni hatari kama likitokea tukio la ghafla, mfano wa moto, litakuwa ni jambo gumu kwao kuweza kujiokoa kupitia ngazi za nje. Hata baadhi ya milango inayotokeza nje ya ngazi hizo katika maghorofa hayo, imefungwa kutokana na ubovu.

Licha ya kero hizo, pia wanafunzi hao walilalamikia kitendo cha kujazana kupita kiasi katika vyumba vyao vya kulala, kwani wamepangwa hadi wanane katika chumba kimoja.

Baada ya kutoka kwenye chumba cha madenti hao (majina tunayo) OFM ilitua kwenye jengo moja ambalo liliwahi kulipuka kwa moto lakini bado limechakaa kutokana na kutofanyiwa ukarabati.

MSEMAJI WA MUHIMBILI ABANWA, AKISALITI CHUO
Baada ya OFM kunasa uozo huo ndipo ilipoamua kuwasiliana na msemaji wa Muhimbili, Amiela Angelekera.

OFM: Habari za leo kiongozi?
AMINIELA: Salama tuu, za kwako? Samahani naongea na nani?
OFM: Unaongea na Operesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ya Global Publishers.
AMINIELA: Ok, nikusaidie nini?
OFM: Unafahamu kama vyoo vya hosteli ya wanafunzi vyote vimejaa? Je, kuna mkakati wowote wa kurekebisha maana ni miezi mingi imepita.
AMINIELA: Mmmh..(anaguna kidogo) sijajua ni vyoo vipi, unatakiwa uwe mwandishi mzuri wa taaluma yako unapozungumzia chuo, njoo twende wote tukaone hivyo vyoo.
OFM: Taaluma ipi ambayo unadhani hawana OFM? Tayari tumefika hapo na kujionea ubovu wa miundombinu ambayo inahatarisha maisha ya wanafunzi na chuo kwa ujumla.
AMINIELA: Nimesema njoo ofisini kwangu, maana sipendi kuzungumza kwenye simu ishu kama hizi, kwanza mimi sihusiki na chuo maana ni taasisi nyingine.
OFM: Ok, kwa nini umelizungumzia suala hilo.
AMINIELA: Sihusiki na chuo, hiyo ni taasisi nyingine.
OFM: Ok, sawa kazi njema.

WAJUA KAMA ZABIBU HUSAIDIA KUTIBU SARATANI NA MARADHI YA MOYO, BASI SOMA HAPA KUJUA ZAIDI

NI kipindi cha kuukaribisha mwaka mpya 2014 na kuuaga 2013. Katika kipindi hiki ni desturi yetu kuwanunulia tuwapendao zawadi na pengine hata kujinunulia wenyewe kama ishara ya kutakiana maisha mema na yenye afya tele.
Kuna zawadi nyingi za kumnunulia umpendae lakini pengine inayoweza kuwa na thamani kubwa na yenye mvuto kwa kipindi hiki ni lishetiba au kwa jina lingine ‘food supplement’ kwa sababu utakuwa umeboresha afya zao baada ya kutumia zawadi hiyo.
Lishetiba zilianza kutengenezwa miaka takribani 50 iliyopita. Hii ilitokana na wanasayansi kubaini kuwa lishe duni ndiyo chanzo cha magonjwa mengi. Wengi waliotumia lishetiba walipona maradhi ya aina mbalimbali.
Mwaka 1994 Baraza la Congress la Marekani liliamua kuweka sheria ya lishetiba (isipokuwa tumbaku na mazao yake) kuwa zitengenezwe, ziuzwe na zitumike chini ya mamlaka na sheria za vyakula.
Pia watengenezaji wa lishetiba walishurutishwa kuweka lebo katika bidhaa zao ikionyesha wazi kuwa si dawa ila ni chakula tu.
Kwa kuwa lishetiba hizo zilizalishwa zaidi ya aina elfu 50, sheria ilitoa maelekezo kuwa lishetiba zote zitumiwe na walaji kupitia mdomoni tu na siyo vinginevyo, awali zilikuwepo mpaka sindano na dripu kama hospitali.
Kadiri dunia inavyoongezeka watu ndivyo fursa ya kupata mlo sahihi inakuwa ngumu na hivyo suala la kujazia upungufu huo kwa kula lishetiba linakuwa ni jambo la lazima.
Kuna aina nyingi za lishetiba, mfano zipo za kuimarisha kinga ya mwili (antioxidant) ambazo zina vitamin C na E, kuna magome ya mkaratusi, juisi ya zabibu ambayo hutoa ahueni kwa wagonjwa wa saratani na wenye maradhi ya moyo, pia imethibitika kuufukuza uzee kwa kufuta makovu na makunyanzi ya uzee huku ikiiacha ngozi iking’ara zaidi na mzee akaonekana kama kijana.
Aidha, zipo lishetiba za ubongo ambazo zimethibitika kuuchachua ubongo wa mlaji na kuimarisha kumbukumbu zake hivyo kuondoa tatizo la  usahaulifu kwa watu wazima na hata wanafunzi. Pia zipo za kuimarisha na kuondoa matatizo kwenye mfumo wa nguvu za uzazi.
Tibalishe zipo za kila aina na kwa kila tatizo, ila hatuwezi kuzitaja zote leo hapa. Tanzania bado ipo nyuma sana katika matumizi ya lishetiba ulinganisha na nchi zingine duniani ambazo zimeweka utaratibu kwa kuuza ‘kila kona’ kuanzia hospitali, maduka ya dawa baridi hadi hotelini na hivyo kufanya upatikanaji wake kuwa rahisi.
Ni ukweli uliowazi kuwa siyo rahisi kupata mlo kamili wenye virutubisho vyote wakati wote, hivyo ni vyema ukajazia upungufu huo kwa kula lishetiba ukiwa na wasaa huo. Sisi kama chombo cha habari tunakuahidi ushirikiano wa dhati katika hili, hivyo usisite kuwasailiana nasi kwa msaada zaidi.

HATARIIII!!!!!! VIDONGE VYA UZAZI WA MPANGO VINACHANGIA MTUMIAJI KUPATA UPOFU, SOMA KWA MAKINI MAKALA HII

Pamoja na kuwa ni njia nzuri ya kuzuia ujauzito, vidonge vya Uzazi wa Mpango vinatajwa kusababisha  ugonjwa wa macho ujulikanao kama Glaucoma, unaoelezwa kuwa ni chanzo kikuu cha upofu.

 Ugonjwa huu unaelezwa kuwa sababu kubwa ya kusababisha upofu kwa wanawake wanaotumia vidonge hivi kwa muda mrefu.

Hayo yamebainishwa kwenye Utafiti wa  Afya na Lishe  uliofanywa na Kituo cha Udhibiti na Uzuiaji wa Magonjwa cha Marekani(CDCP).

Utafiti huo unasema kuwa, seli zilizoko katika neva za macho zina homoni za estrogen  ambazo hufanya kazi ya kulinda macho, vidonge hivyo huingilia mchakato  huo wa ulinzi kwa kupunguza kiwango cha homoni hizo.

Unasema kuwa wanawake wanaofunga hedhi mapema au wanaotumia vidonge ambavyo huzuia kuzalishwa kwa vichocheo vya estrogen, na dawa za saratani ya matiti, huweza kupata upofu.

Wanawake zaidi  ya 3,400  wenye umri wa zaidi ya miaka 40 walifuatiliwa kwa zaidi ya miaka mitano ikiwa ni sehemu ya utafiti huo.

Profesa Shan Lin wa Chuo Kikuu cha Carlifonia, San Francisco anasema wanawake wanaotumia vidonge hivyo kwa zaidi ya miaka mitatu, wanatakiwa kupima maradhi ya macho aina ya Glaucoma na afya zao zifuatiliwe kwa uangalifu na wataalamu wa macho.

Utafiti huo umebaini kuwa wanawake waliotumia vidonge hivyo kwa miaka zaidi ya mitatu walikuwa na hatari kwa asilimia tano ya kupata upofu usababishwao na glaucoma ukilinganisha na wasiotumia vidonge  hivyo.

 Kiongozi wa utafiti huo, Dk Louis Pasquale  wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Havard anasema vichocheo vya Estrogen  vina umuhimu katika  seli za retina ambazo zinajulikana kwa kupokea homoni hizo.

“Kuwepo kwa homoni za estrogen kunazisaidia seli hizo kuwa hai kwa hiyo wanawake wanapotumia vidonge vya uzazi, homoni hizo huharibiwa na kurahisisha uharibifu wa macho,” anasema Dk Pasquale.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, Dk Cyriel Masawe wa Chuo  Kikuu cha Tiba cha Muhimbili (MNH) anasema  ni hatari kwa wasichana wadogo ambao hawajaolewa kutumia dawa hizo ovyo.

“Kwa mfano mikoa ya Lindi na Mtwara, tumegundua wasichana wadogo ambao hawajaolewa wanatumia zaidi sindano za uzazi wa mpango na vidonge,” anasema
Dk Masawe anasema si vyema watu kuzitumia dawa za Uzazi wa Mpango kwa  mazoea na endapo wataona ni vyema kufanya hivyo, washauriane na wataalamu wa afya.
Anasema  kuwa elimu inahitajika kwa kina kuhusu matumizi ya dawa hizo kwani wapo baadhi ya watu wanaozitumia bila mpangilio wala utaratibu maalum.
“Hizi dawa zinasaidia lakini zisipotumiwa kwa uangalifu, huenda zikasababisha madhara,” anasema Dk Masawe.
Kwa upande wa utafiti huo uliojikita kuangalia madhara ya vidonge hivyo kwa wanawake, watu wanaovitumia wanatakiwa kuwa makini na uhusiano uliopo kati ya afya ya uzazi na maradhi ya macho hasa kama mtumiaji amefunga hedhi mapema.
Matokeo ya utafiti huo yaliyotolewa katika mkutano wa kila mwaka wa Chuo Kikuu cha Mfumo wa Macho Marekani (USP), yanasema wanawake zaidi ya 3,046 walifanyiwa uchunguzi kuhusu afya ya uzazi na maradhi ya macho.
 Pamoja na sababu nyingine za maradhi ya macho,  wanasayansi waliofanya utafiti huo wanasema kutumia vidonge vya uzazi kwa muda mrefu, ndicho chanzo kikuu cha upofu na kutaja sababu nyingine kuwa ni historia ya familia, shinikizo la ya macho na kisukari.
 Watalaamu wa afya nchini wanasema bado madhara ya dawa hizo yanatofautiana kulingana na aina ya dawa anayotumia mhusika.
Madhara mengine ya dawa hizi ni pamoja na kichefuchefu, kichwa kuuma, matiti  kuuma, kuongezeka uzito na kupata hedhi bila mpangilio.
Dk Joseph Matiku wa Kituo cha Afya, Mugumu, Serengeti anasema, hatari zaidi ni kwa binti wanaotumia dawa hizo kwa muda mrefu kabla hawajaanza maisha ya ndoa.
“Wapo wanawake ambao wanapata uvimbe kwenye kizazi kutokana na matumizi ya muda mrefu ya dawa hizi. Ingawa hakuna utafiti uliofanyika kuthibitisha hili, lakini wanawake wengi wanaotumia dawa hizi hapa nchini wanapata uvimbe maarufu wa Fibroids” anasema.
Hata hivyo, Oktoba mwaka huu, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi anasema Wizara ya Afya ipo kwenye harakati za kutafuta fedha ili kuhakikisha asilimia 60 ya wanawake wanaostahili kupanga uzazi wanapata dawa husika.
Mwaka jana wakati wa Mkutano wa Uzazi wa Mpango uliofanyika London Uingereza, Rais Jakaya Kikwete aliahidi kuwa hadi kufikia mwaka 2015 Tanzania itafikisha asilimia 60 katika huduma za uzazi wa mpango.
Vilevile katika Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Uzazi wa Mpango uliofanyika Oktoba mwaka huu, Makamu  wa Rais Dk Gharib Bilal alisema juhudi za ziada zinahitajika kuhakikisha kiwango cha watumiaji wa huduma za uzazi wa mpango, kinaongezeka ili kutimiza lengo la kimataifa ya kuongeza idadi ya watumiaji wa huduma hiyo.
Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), zinaonyesha kuwa, kiwango cha matumizi ya huduma za uzazi wa mpango kwa nchi zilizoendelea ni asilimia 72, huku Tanzania iliyo kwenye kundi ya nchi zinazoendelea ikiwa ni asilimia 27 tu.
 Dawa za uzazi wa mpango hufanyaje kazi?
Vidonge vya uzazi wa mpango hufanya kazi ya kuweka uwiano  katika kiwango cha vichocheo.
Katika hili, kazi kubwa ni kuzuia homoni za estrogen kuongezeka na kufikia kiwango cha kati au cha juu.
 Bila homoni ya estrogen, tezi ya pituitari haiwezi kuifanya mirija ya uzazi kuruhusu mayai yaliyochavushwa kwenda kukutana na mbegu za kiume kwa ajili ya utungishwaji wa mimba.

KASI YA MAAMBUKIZI YA UKIMWI SASA YASHIKA KASI ZANZIBAR.


RAIS wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein anatazamiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yatakayofanyika Paje Mkoa wa Kusini Unguja .
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kamishina ya Ukimwi Zanzibar (ZAC) Dk Omar Shauri Makame .

Katika mkutano wake na waandishi wa habari alisema kwamba maadhimisho ya mwaka huu yanafanyika wakati kunaonekana kuwapo na ongezeko la maambukizi mapya.
Alisema katika mwaka 2012-2013 watu 108 walikutwa na maambukizi mapya na kufanya idadi ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi kufikia 6,125 kwa mujibu wa takwimu za watu waliofika katika vituo vya afya kuchunguza afya zao ikiwemo damu.

“Utafiti wa takwimu za ugonjwa wa Ukimwi zinaonesha kwamba yapo maambukizi mapya ya ugonjwa huo kwa kiwango kikubwa ambapo juhudi za makusudi zinahitajika,”alisema.

Kwa mfano alisema Tume ya Ukimwi imeweka mikakati kuyadhibiti makundi hatarishi ikiwemo vijana wanaotumia dawa za kulevya ambapo maambukizi ya kundi hilo yapo kwa asilimia 25.

Mapema Dk Shauri aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya Siku ya Ukimwi wiki ijayo ambapo ujumbe ni mapambano ya Ukimwi kwa wote yakiwa na lengo la kuwashirikisha watu wenye rika tofauti.
Maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi kwa Zanzibar yapo kwa asilimia 14 kwa zaidi ya miaka mitano sasa.

MWANAUME MWENYE MOYO ULIO OTEA TUMBONI, SOMA ZAIDI HAPA


Ho Zhiliang, 24, raia wa China amezaliwa huku moyo wake ukiwa unaota maeneo ya tumboni kama unavyo ona kwenye picha. Kijana huyu ana subiri upasuaji ili kuweza kurekebisha kiungo hicho na kukirudisha mahali kinapotakiwa kuwa.


Kweli Mungu ni wa ajabu sana maana inasemekana watoto wengi wanao zaliwa na tatizo hili hufa siku chache baada ya kuzaliwa lakini imekuwa tofauti kwa huyu kijana ambaye ni kinyozi na ameamua kuishi maisha yake na hali hiyo hadi pale alipo soma kwenye gazeti moja kwamba hali hiyo inaweza rekebishwa kwa opareshi ambayo ndo anasubiria.

Hii si kesi ya kwanza kutokea huko China.

AATHIRIKA KWA KANSA YA MATITI, ONA JINSI ILIVYOMUHARIBU VIBAYA, NENDA HOSPITALI KAPIME ILI UJUE KAMA UNAYO ILI UANZE MATIBABU MAPEMA






Idiagbonya Osarere Debbie is a medical technician who is suffering from 4th grade Invasive Ductal Carcinoma - cancer of the breast and its spreading really really fast. One of the breasts is condenmed already and it has moved to the second breast and her neck. She desperately needs N6 million for surgery and her family and friends say that she has barely one month more to live without surgery.





Please please, donate to debbie, no matter how small, please. Continue to see photos of Debbi's condition right now.








 
 
 

FAHAMU JINSI UGONJWA WA KISUKARI UNAVYOSABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA UGONJWA WA FIGO

 
Watu wenye kisukari, wanashauriwa kufanya uchunguzi wa figo zao mara moja kwa mwaka ambapo utachunguzwa kama una dalili zozote zinazoashiria matatizo ya figo. Utapimwa mkojo kwa ajili ya kuchunguza kiwango cha protini iitwayo Albumin au Microalbuminuria.
Kabla ya kuanza kueleza matibabu ya matatizo haya nikumbushe kwa kusema kuwa kuwepo kwa kiasi kingi cha protini katika mkojo ni mojawapo ya dalili za kuwepo kwa tatizo katika figo.
Mgonjwa wa maradhi haya ni lazima katika vipimo atakavyofanya daktari aangalie  kiasi cha Urea Nitrogen katika damu (BUN), kiwango cha Creatine katika damu (serum creatinine) na kiasi cha protini katika mkojo wa saa 24 (24-hour urine protein).

Kabla ya kufafanua tiba ni muhimu kukumbusha pia kuwa ni vyema mgonjwa akaangaliwa kiasi cha madini ya Phosphorus, Calcium, Bicarbonate, PTH, na Potassium katika damu.
Itakuwa vema kama daktari ataangalia kiasi cha wingi wa damu (Haemoglobin), na wakati fulani kufanya Biopsy ya figo kwa ajili ya uthibitisho wa tatizo.

Matibabu
Matibabu ya ugonjwa wa figo unaotokana na kisukari ni muhimu sana kufanyika haraka baada ya dalili kujitokeza. Lengo kuu la matibabu ni kufanya figo zisiendelee kuathirika. Mojawapo ya njia bora kabisa za kusaidia hilo ni kudhibiti kiwango cha shinikizo la damu kuwa chini ya 130/80 mmHg.

Zipo dawa ambazo husaidia tatizo hili kama vile zile za jamii ya Angiotensin Converting Enzyme Inhibitors kwa mfano Captopril pamoja na zile za Angiotensin Receptor Blockers zimeonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kushusha shinikizo la damu wakati huohuo kudhibiti kasi ya kuharibika kwa figo kutokana na kisukari.
USHAURI
Wagonjwa wanashauriwa kula lishe yenye kiwango kidogo cha mafuta, matumizi ya dawa za kudhibiti kiasi cha mafuta mwilini, na kufanya mazoezi mara kwa mara kama vile kutembea kwa saa mbili na wawe wanakunywa maji kwa wingi kabla na baada ya matembezi kwani husaidia sana kuzuia au kupunguza kasi ya kuathirika kwa figo.

Wagonjwa wanashauriwa kubadilisha aina ya chakula wanachokula, kutumia dawa za kisukari kama inavyoshauriwa na daktari na kuchunguza kiwango  cha sukari kila mara kwani husaidia kuzuia tatizo hili.
Waliopatwa na ugonjwa wa kisukari wanaweza kuwa na chombo cha kujipima wenyewe kiwango cha sukari mwilini mwao, ugonjwa huu huchangia sana kuua nguvu za kiume.

MTOTO MWENYE UGONJWA WA AJABU APELEKWA INDIA KUTIBIWA, TUMUOMBEE KWA MUNGU

Mtoto Seleman Rajabu (16) ambaye mguu wake ulianza kuvimba wenyewe tangu alipozaliwa.
Stori: Imelda Mtema
MTOTO Seleman Rajabu (16) ambaye mguu wake ulianza kuvimba wenyewe tangu alipozaliwa, amechangiwa fedha zaidi ya Sh. Mil. 4 ambazo zimemwezesha kwenda nchini India kupata matibabu.

Akizungumza na mwandishi wetu, kijana huyo alisema hana chochote cha kuwalipa Watanzania waliojitolea kumsaidia, bali atawaombea kwa Mungu ili awabariki kwani maumivu ya mguu wake yanampa mateso makubwa.
“Nawashukuru sana wote walionichangia kwa moyo wao wa huruma na kuona ni jinsi gani ninateseka kila siku, nitazidi kuwaombea kwa Mungu wazidi kufanikiwa zaidi,” alisema Sele.
Zaidi aliishukuru Kampuni ya Global Publishers Ltd kwa kuendesha kampeni ya kumchangia kupitia magazeti yake ya Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani na Ijumaa kwani kupitia magazeti hayo, Watanzania wengi waliweza kuguswa na tatizo lake na kujitolea kumchangia.
Seleman hakusita pia kumpongeza mtangazaji wa Kipindi cha Mimi na Tanzania kinachorushwa kupitia Runinga ya Channel Ten, Hoyce Temu kwa kumpa fursa ya kumuonyesha katika kipindi chake ambacho pia kimetoa fursa ya watu kumchangia.
“Namshukuru sana dada Hoyce Temu na Mungu azidi kumbariki maana kipindi chake pia kimenisaidia sana msaada wa kuniwezesha kuanza kupata matibabu,” alisema.
Akizungumzia safari hiyo ya India, mtoto huyo alisema kila kitu kinakwenda vizuri, tayari ameshaanza taratibu za kukatiwa viza ambapo anatarajia kuanza safari wiki ijayo.

Seleman alianza kuugua tangu azaliwe, mguu ulianza kuvimba taratibu, ukaendelea kukua pasipo kujulikana sababu ambapo mwishoni alipelekwa katika Hospitali ya CCBRT, jijini Dar ambao walishauri mguu huo ukatwe, mama yake akakataa na kuitisha harambee ya kuchangiwa.
-GPL

UJUE UGONJWA HATARI WA HEPATITIS B UPO

Mgonjwa mwenye Hepatitis B ngozi na macho yake vikiwa vya njano.
HEPATITIS B NI NINI?
Hepatitis B ni ugonjwa wa manjano ambao hushambulia ini.
Ugonjwa huu kama haujatibiwa hutengeneza uvimbe katika ini na kusababisha kansa ya ini na baadaye KIFO.
Inakadiriwa watu milioni 350 duniani wameathirika na ugonjwa huu ambapo watu 620,000 hupoteza maisha kila mwaka kwa ugonjwa huu.

HEPATITIS B UNASABABISHWA NA NINI?
Ugonjwa huu husababishwa na virusi waitwao Hepatitis B (HBV) ambao hukaa katika ini, damu na baadhi ya majimaji mwilini.

Virusi vya Hepatitis baada ya kulishambulia ini.
UNAAMBUKIZWAJE?
Ugonjwa huu huambukizwa kwa njia zifuatazo:
-Kujamiana bila kinga
-Kunyonyana ndimi
-Mama mwenye ugonjwa kumwambukiza mtoto wakati wa kujifungua
-Kuchangia damu isiyo salama
-Kuchangia vitu vya ncha kali kama sindano, wembe n.k
-Kuchangia miswaki

Mojawapo ya njia zinazoambukiza ugonjwa wa Hepatitis B.
NB: Ugonjwa huu hauambukizwi kupitia chakula, maji au kushikana mikono na waathirika.
DALILI ZAKE
Dalili za ugonjwa huu huchukua muda mrefu kuonekana, zikionekana mgonjwa anakuwa tayari ameathirika sana na ni kama ifuatavyo:

-Uchovu
-Kichefuchefu
-Mwili kuwa dhaifu
-Homa kali
-Kupoteza hamu ya kula
-Kupungua uzito
-Maumivu makali ya tumbo upande wa ini
-Macho na ngozi kuwa vya njano
-Mkojo mweusi

Daktari akifavya vipimo vya ugonjwa wa Hepatitis B.
KINGA
-Chanjo
-Kutumia kinga wakati wa kujamiana
-Kuacha kuchangia vitu vya ncha kali kama sindano, wembe n.k
-Kutochangia miswaki
-Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu
-Kutochangia damu isiyo salama

Mgonjwa wa Hepatitis B akipandikizwa ini na madaktari.
TIBA
-UGONJWA HUU HAUNA TIBA, japo mgonjwa akiwahi hospitali atapatiwa dawa za kupambana na virusi kuvipunguza nguvu za kushambulia ini.
-Kupandikiza ini ambapo ini lililoathirika huondolewa na kuwekwa ini lingine japo ni vigumu kupata ini salama.
-Mgonjwa anashauriwa kuacha kutumia pombe, madawa ya kulevya na vitu vingine vinavyochosha ini.

YAJUE MAUMIVU YA KORODANI (TESTICULAR PAINS)


Kwa kawaida maumivu ya korodani hupanda juu zaidi na kuacha mfuko wake mtupu.  Tatizo hili huwatokea zaidi vijana chini ya umri wa miaka 25 ingawa pia inaweza kutokea katika umri zaidi ya huo. Tatizo hili huhitaji upasuaji wa dharura.
Wakati mwingine tatizo hili hutokea kwa korodani kuwa na tabia ya kupanda au kushuka, ikishuka mgonjwa hupata nafuu, hali huendelea vivyohivyo kwa vipindi fulani. Hali hii inapotokea mgonjwa hutapika na kukosa nguvu.

Maambuziki ya korodani pia mtakuja kuyaona kwa undani baadaye lakini pia huambatana na maambukizi katika mkojo au ‘UTI’ na homa. Huwa makali kwa vipindi. Kisonono na gono huchangia tatizo hili kwa kiasi kikubwa.
Uvimbe kama jipu wa korodani au Fonias gangrini kama tulivyoona hapo awali ni mbaya kwani korodani inakuwa kama inaoza halafu tatizo hilo lina tabia ya kusambaa kuelekea uvunguni jirani na njia ya haja kubwa. Uvimbe huwa kama busha au jipu kubwa lakini ndani yake hakuna maji wala usaha.
Tatizo hili pia tutakuja kuliona kwa undani kwani nalo huathiri wanaume wengi na ni tatizo kubwa ambalo mwanaume yeyote ni rahisi kupata pia hupoteza uwezo wa kuzaa.
KORODANI KUSHINDWA KUFANYA KAZI (TEST CULAR FAILURE)
Kazi ya korodani ni kuzalisha  vichocheo au homoni za kiume na mbegu za kiume. Mwanaume anatakiwa awe na korodan mbili ingawa ukiwa na moja pia inaweza kufanya kazi kama ni nzima, inatakiwa kama unayo moja nenda hospitali ukapimwe kuthibitisha ubora wake na uwezo wake.

Katika hali isiyo ya kawaida wapo wanaume wenye korodani tatu.
Ukishakuwa  na hali hii ni vema ukapimwe hospitali.
Matatizo mengi ya korodani tumeshayaona kwa kina  katika matoleo  yaliyopita na tunamalizia kuyaona leo huku tukiangalia na mada hii.

Matatizo ya korodani kama tulivyoyaona ndiyo matokeo ya kushindwa kufaya kazi.
Korodani kushindwa kufanya kazi tunaweza kuweka katika makundi mawili, kwanza ni hali ya uwezo wake kuwa mdogo tangu balehe ‘Hypogonadism’ na tatizo linaweza kutokea ukubwani yaani baada ya  balehe au utu uzima ‘secondary hyponadism.’

Tatizo linapotokea katika utu uzima huambatana na upungufu wa nguvu za kiume, kusinyaa korodani na uume kuwa mfupi au mdogo. Hii ni kutokana na korodani kushindwa kuzalisha vichocheo au homoni za kiume kama tatizo ni tangu balehe, basi hali ya matatizo makubwa hutokea katika mfumo wa uzazi na mwili kwa ujumla. Hayo ni baadhi tu ya matatizo ila mengi tutaendelea kuyaona.
CHANZO CHA TATIZO
Korodani kushindwa kufanya kazi husababishwa na matatizo mengi kama vile matumizi ya madawa baadhi yake ya hospitali kwa muda mrefu hasa kwa wanaume mfano dawa za jamii ya Glucocorticoids, Ketoconazole, na  madawa ya kulevya hasa bangi.

Matatizo ya kuzaliwa nayo Chromosome Problems magonjwa yanayoathiri korodani mfano Mumps na joto kali na la muda mrefu katika korodan. Kuumia moja kwa moja kwa korodani Direct Injury na kuvimba na kujinyonga kwa korodani Testicular Torsion.
Watu ambao wapo katika hatari kubwa korodani zao kuja kushindwa kufanya kazi ni wale ambao hufanya shughuli zinazoumiza korodani zao taratibu na kwa muda  mrefu mfano waendesha pikipiki au bodaboda katika barabara mbovu kwa muda mrefu, huwa kitaalamu huziumiza korodani zao Constant low level injury to the Scrotum na wale ambao wana korodani moja au hawana kabisa.
DALILI ZA TATIZO
Endapo korodani zako zinashindwa kuzalisha mbegu za kiume utajikuta unaishi na mke kwa zaidi ya mwaka mmoja na mnafanya tendo la ndoa kwa lengo la kutafuta mtoto na mnakosa.

Endapo korodani zinashindwa kuzalisha homoni za kiume basi utakuwa na dalili zifuatazo, kama ni mtoto anakuwa harefuki anaendelea kuwa mfupi huku umri unaenda, matiti ya mtoto wa kiume au kijana yanakuwa makubwa Gynecomastia mwili hauwi na misuli imara, kukosa hamu ya tendo la ndoa, unakuta vinyweleo vya kwapani na sehemu za siri havioti au kama vilishaanza kuota havikui hata kwa zaidi ya mwaka, huoti ndevu na kubadilika kama mwanaume, uume haukui na korodani zinasinyaa na kuwa kama za mtoto. Sauti haiwi nzito.
UCHUNGUZI
Matatizo ya viungo vya uzazi huchunguzwa katika hospitali za wilaya na mkoa, uchunguzi wa awali hufanyika kwenye vituo vya afya.
Vipimo mbalimbali hufanyika kadiri daktari atakavyoona inafaa.

USHAURI
Matibabu huchukua muda mrefu baada ya uchunguzi wa kina. Matibabu ya dharura hufanyika pale kunapokuwa na maumivu makali.
Ni vema kuepuka maambukizi hasa ya magonjwa ya zinaa na kuwahi hospitali pale unapohisi una tatizo.

GHARAMA ZA MATIBABU MUHIMBILI ZAPANDA MARADUFU

Gharama za huduma  za kulipia matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili zimepanda maradufu.
Hatua hiyo inayotekelezwa bila kuwashirikisha wadau na watoa huduma ilianza Septemba mosi mwaka huu na kulalamikiwa na wagonjwa na wafanyakazi.

Kwa mujibu wa tangazo la Mkurugenzi wa MNH, lililobandikwa kwenye ubao wa matangazo wa jengo la mateniti la kulipia huduma  IPPM, inaonyesha kuwa gharama zilipanda kuanzia Septemba 2, wakati notisi hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi ilitolewa Septemba 4.

Wagonjwa wanaolipia matibabu  binafsi Muhimbili  waliliambia gazeti hili kuwa  wateja wanaotumia ‘ast truck’  na huduma ya uzazi inayotolewa na  kitengo cha mateniti- IPPM ndizo zilizoongezeka.
  
Kuanzia sasa upasuaji wazazi  unalipiwa Sh. 500,000 badala ya  350,000 za awali. Uzazi  wa kawaida  ni Sh. 250,000 badala ya  Sh. 150,000  zilizokuwa zikitozwa mwanzo.

Walisema kulala kunagharimu  Sh. 20,000  badala ya 15,000 wakati tozo la kumuona daktari kwa mara ya kwanza  ni Sh. 30,000 badala ya Sh. 20,000 za awali.   

Kumuona daktari kwa ajili ya kufuatilia huduma na matibabu zimepanda hadi Sh. 20,000 kutoka Sh. 10,000.

Huduma nyingine kama dawa na uchunguzi wa maabara  
zimepanda japo bei zake hazikutangazwa  kwenye ubao wa matangazo.

Kwa wagonjwa wa kujifungua kawaida ambao  hawalipii gharama  watatozwa gharama ambazo hazikafafanuliwa ingawaje serikali inataka watibiwe bure.

“Mfano mjamzito akipata uchungu ghafla na kufika Muhimbili bila rufaa atatakiwa kalipia gharama” alisema mjamzito jina tunalo.

Msemaji wa MNH Aminieli Aligaesha, alikiri kuongezeka gharama hizo ziliongezeka  na kuongeza kuwa sababu ya ongezeko  hilo ni gharama kubwa za uendeshaji.

Hata hivyo alikataa kutoa maelezo zaidi na kutaka mwandishi wetu kwenda ofisini kwake   kwa maelezo zaidi.

Hospitali ya Muhimbili inatoa huduma kwa utaratibu wa aina mbili kuchangia matibabu kunakofanywa na mgonjwa wa rufani pamoja na serikali.

Njia nyingine ni  wagonjwa kulipia gharama zote  za tiba kama ambavyo wanafanya kwenye hospitali za binafsi. 

Hata hivyo gharama za tiba kwa wale wanaochangia matibabu na wale wa rufaa hazijaongezeka

ZIJUE SIKU ZA KUPATA MIMBA




Leo napenda nizungumzie jambo moja tu ambalo ni juu ya 
jambo moja tu, nalo ni namna wanavyoweza kui-pin point siku ile ya kilele (i.e fruitful/productive/fertile 
day), hapa nina maana ya siku ile ambayo wao wanaiita siku ya 14.  

Ikumbukwe kuwa wanawake wanatofautiana katika suala zima la urefu wa MENSTRAL CYCLE, yaani 
idadi ya siku kati ya period ya kwanza hadi ile ya pili inayofuatia. Kundi kubwa la wanawake wana fall 
kwenye range ya siku 22-35. Japo walio-normal wana siku 28. Vile vile kuna wengine huwa na menstral 
cycle mbili, yaani fupi na ndefu. Hivyo walio na menstral cycle fupi, mathalani wale wenye siku 22, huwa 
vilevile wana kipindi kifupi sana cha kutokwa na damu (period), yaani damu inaweza kukatika ndani ya 
siku 2 tu! Na wale wenye siku 35 au zaidi huwa wana kipindi kirefu sana cha kutokwa na damu (period) 
ambapo wengine huwachukua hata siku kati ya 5 hadi 8.  

Hivo basi, kama wewe ni mwanaume inakubidi umwelewe vizuri mwenzi wako juu ya hayo niliyoyasema 
hapo juu ili ikusaidie kui-pin point ile fertile day (yaani siku ya mimba).  

Swali: Je siku ya mimba ni ipi? 

Jibu lisilosahihi: Watu wengi na hata baadhi ya wanasayansi wanafikiri siku ya mimba ni ile ya 14 baada 
ya dalili za kwanza za damu ya hedhi! Wao huhesabu kuanzia siku ile damu ilipoanza kutoka hadi siku ya 
14! Utaratibu huu ume-prove failure! Hii ni kwa sababu wanawake wana menstral cycle 
zinazotofautiana kwa urefu. Hivo basi jibu sahihi ni hili hapa chini: 

Jibu sahihi:  
1. Kwanza inabidi ujue kama mwenzi wako ana menstral cycle ipi? Fupi au ndefu, ama zote mbili? 

2. Baada ya kujua urefu wa menstral cycle ya mwenzi wako then pin point siku ile ya mwisho halafu 
uhesabu backwards siku 15 kuanzia siku ile ya mwisho. Siku hii ya 15 kuanzia mwisho ndiyo siku ya 
mimba kwa mwanamke yeyote!  

Once you know the '15th day' from the last one, then you can manoeuvre whatever you want to get her 
pregnant or to avoid pregnancy!  

With this new approach of pin pointing the fertile day you will find that all women (menstral cycles) 
are covered, whereas the old way of counting fits only to women whose menstral cycles are 28 days! 


Naomba nitoe mifano hai kwa faida ya dada zetu na wengine: 

1. Kama mwanamke ana menstration cycle ya siku 22 inabidi afanye kama ifuatavo: Kwanza 
itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama hapa 
chini: 

1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th, 
20th, 21st, 22nd. 

Kisha ahesabu kuanzia ile 22nd day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15. Ataona kuwa siku ya 
kumi na tano inaangukia kwenye 8th day ya kalenda yake. Hivo 8th day ndiyo siku ya mimba 
kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 22. Akumbuke kwamba 1st day 
ndiyo siku anayoanza ku-bleed! 


2. Kama mwanamke ana menstration cycle ya siku 28 inabidi afanye kama ifuatavo: Kwanza 
itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama hapa 
chini:  

1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th, 
20th, 21st, 22nd, 23rd, 24th, 25th, 26th, 27th, 28th. 

Kisha ahesabu kuanzia ile 28th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15. Ataona kuwa siku ya 
kumi na tano inaangukia kwenye 14th day. Inamaana kwamba 14th day ndiyo siku ya mimba 
kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 28. Akumbuke kwamba 1st day 
ndiyo siku anayoanza ku-bleed! 


3. Kama mwanamke ana menstration cycle ya siku 35 inabidi afanye kama ifuatavo: Kwanza 
itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama hapa 
chini:  

1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th, 
20th, 21st, 22nd, 23rd, 24th, 25th, 26th, 27th, 28th, 29th, 30th, 31st, 32nd, 33rd, 34th, 35th. 

Kisha ahesabu kuanzia ile 28th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15. Ataona kuwa siku ya 
kumi na tano inaangukia kwenye 21st day. Inamaana kwamba 21st day ndiyo siku ya mimba kwa 
mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 35. Akumbuke kwamba 1st day ndiyo 
siku anayoanza ku-bleed! 


4. Kama mwanamke ana abnormal menstration cycle ya siku 15 , BASI KUNAUWEZEKANO 
WA KUTOPATA MIMBA KABISA KAMA INAVYOONEKANA HAPA CHINI:  

Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama 
kawaida:  

1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th. 

Kisha ahesabu kuanzia ile 15th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15. Ataona kuwa siku ya 
kumi na tano inaangukia kwenye 1st day. Inamaana kwamba, the 1st day of her bleedind ndiyo 
siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 15. Akumbuke 
kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed, na ndiyo hiyo hiyo siku ambayo mwanamke wa 
kundi hili anaweza kupata mimba! 

Hii inamaana kwamba, siku ambayo linaharibika lile yai la upande mmoja ndiyo siku hiyo hiyo 
ambayo yai la upande wa pili linapevuka tayari kwa kurutubishwa. Mwanamke wa aina hii 
anaweza kupata mimba tu kama atakutana na mwanaume siku ile anayoanza kubleed, kwani siku 
ambayo yai moja linaanza kuharibika ndio siku hiyo hiyo ambayo yai la upande wa pili 
linakuwa tayari kurutubishwa! 

Na wanawake wa kundi hili la nne ukiwauliza vizuri watakiri kwamba hawajawahi kuona au ku-feel ule ute mweupe ambao wenzao huwa wanaupata siku ile yai linapokuwa tayari kwa 
kurutubishwa, kwani ute wa wanawake wa kundi hili la nne huwa unachanganyikana na damu 
kwa vile unatoka siku ile ile wanapoanza ku-bleed. Pia wanawake wa kundi hili huwa 
wanatokwa na kiasi kidogo sana cha damu; na bleed hukatika ndani ya siku moja au mbili tu!  

Jambo la kushangaza ni kwamba, wanawake wengi hawana knowledge ya kutosha juu ya hili 
suala la siku ya mimba; hasa wale ambao wana menstration cycle inayobadilikabadilika! Wao 
husitukia tu wameanza ku-bleed. Ndo maana hawawezi hata ku-plan kutopata mimba! Hawana 
ujanja kabisa ndio sababu wengi wanatumia sindano na njia zingine nyingi za artificial ambazo 
mwisho wa siku huwaletea matatizo ya uzazi, kwani nyingi hu-block njia ya uzazi! Nimeona 
wengi wenye matatizo ya uzazi unaosababishwa na hizi artificial family planning. Wengine 
hulazimika kwenda hospital kuzibuliwa ili wapate mimba jambo ambalo ni hatari kwa afya zao! 
Full maelezo ya kujitosheleza, ukikosa kudaka au kudakisha mimba basi kuna walakini