FAHAMU NGUVU YA M1 NDANI YA CHADEMA.

WAKATI Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),ikizidi kuumiza vichwa kuhusu mtu wa wapili aliyekuwa katika mikakati ya mapinduzi ya waraka wa mabadiliko ya Chama hicho kama inavyoitwa na viongozi wakuu kuwa ni waraka wa mapinduzi ya Chama.

Katika mkakati huo wa mapinduzi ya Mwenyekiti wa Chadema Kitaifa, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wake Dk Willbrod Slaa, wahusika pamoja na walengwa wa kuchukuwa nafasi hizo waliwekwa katika makundi wawili yenye watu wawili waili, huku kundi la kwanza likiwa ni M2 na M3 wakati kundi la pili likiwa na majina ya M1 na MM kwa maana ya Mhusika Mkuu.

Tayari M3 ameshajulikana kuwa ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha Samson Mwigamba, wakati M2 akiwa ni Dk Kitilia Mkumbo na MM akiwa ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, huku kitendawili ikibaki kwa M1 ambaye mpaka hivi sasa ajajulikana, hatua hiyo imeelezwa kwamba ni pigo kubwa Chadema, kwa sababu inaaminika kwamba hali hiyo bado ni pigo kubwa kwao, kwani haijawa dawa ya kuzuia mapinduzi hayo kwa sababu haijuliknani kuwa M1 ana nafasi gani ndani ya Chama na anaiingia katika kamati na vikao vipi vya muhimu ndani ya Chama hicho.

Hata hivyo Mdadisimambo.blogspot.com imefanikiwa kupata jina la M1 pamoja na wadhifa wake ndani ya Chama hicho Kikuu cha Upinzani Tanzania, M1 ni kati ya watu wenye ushawishi mkubwa ndani ya Chama hicho na anaingia katika vikao muhimu vya maamuzi mazito ndani ya Chama, hata katika vikao vya Kamati vilivyomalizika kwa maamuzi mazito alikuwepo na kushiriki kwa asilimia 100 katika mchakato mzima.

"Huyu M1 ndiyo mtu pekee aliyebaki ndani ya Chadema ambaye anaweza kutusaidia kufanya mikakati yetu kuanzia sasa hadi Uchaguu Mkuu wa Chama utakapofanyika hapo mwezi wa sita mwakani,ingawa hatujamwambia lakini tunajiandaa kumwambia kwa sababu awali tulikuwa tukisubiri barua ya mashtaka yetu"kilisema chanzo chetu.

Moja ya nukuu katika waraka huo ulifafanua kwamba, "Tulikubaliana kwa kauli moja kwamba katika kutekeleza mkakati huu tunahitaji members hawa wawe wametulia kimaisha. Inakuwa vigumu kwa mfano kumtaka member aende mahali fulani kwa makusudi ya mkakati huu wakati hajui familia yake nyumbani anaiacha inakula nini. Tuliona kwamba M3 tayari hana kazi kwa sasa tena kwa kufanyiziwa na wakuu waliopo";

"Ni katika mwendelezo huo huo tunamwona M2 naye akiwa ukingoni kupigwa nje na kuachwa mtupu na wakuu waliopo katika kile wanachokiita wao reshuffle ya ofisi kuu.Kwa sababu hiyo tukapendekeza kwamba MM kwa kushirikiana na M1 kwa hatua ya kwanza wanaweza kutafuta kiasi cha sh. 2m kila mmoja tukijua kwamba kama members hawa wawili wakisaidiwa milioni mbili mbili wanaweza kuanzisha projects ambazo zitawasustain hata kama hawana ajira.

 Kwa hatua ya baadaye tutasaidiana kuona kama hawa members wanaweza kusecure good employments mahali, provided hazitawazuia kufanya siasa".