HIVI MTU AKIFARIKI SALIO LAKE LA PESA LILILOPO KWENYE SIMU (M PESA, TIGO PESA NA MITANDAO MINGINE) LINAKWENDA WAPI, NAOMBENI WADAU MNIAMBIE

Kutokana na makampuni karibu yote ya simu Tanzania kuwa na huduma hizi za mobile money, Je inapotokea mteja amefariki, makampuni yanawajibika vipi kuhusu kurudisha pesa za mteja wao kwa msimamizi wa mirathi au warithi?

swali hiili linazingatia kuwa wateja wanaoweza kutwa na mauti kwa vyovyote wanaweza kuwa na akiba kidogo kwenye ac zao za mitandao ya simu wanayotumia!

Je kuna sheria yoyote ambayo imeweka bayana masuala haya?

kwa wenzetu walio kwenye makampuni ya simu tafadhali mtusaidie kwa hili!
naomba kuwasilisha kwa mjadala!