VIDEO: MANCHESTER UNITED ALIWA TENA, SAFARI HII ALIWA NA NEWCASTLE MOJA KWA BILA (0-1), ANGALIA GOLI HAPA

Manchester United imeendelea kuwa na msimu mbaya baada ya kupigwa bao 1-0 katika mechi iliyomalizika muda mfupi uliopita kwenye Uwanja wa Old Trafford wakati ilipokuwa ikipambana na Newcastle United katika mchezo wa Premier.
Kipingo hicho ambacho ni cha tano kimeifanya Man United iwe na msimu mbaya kuliko yote ndani ya kipindi cha miaka 20 iliyopita, ambapo Jumatano iliyopita, United ilifungwa bao 1-0 na Everton katika ligi hiyo.
Bao la Newcastle lilifungwa na Yohan Cabaye katika dakika ya 61.