Mahaba mahabani! Staa wa sinema za Kibongo,
Chuchu Hans amefunguka kuwa staa mwenzake ambaye ni mwandani wake,
Vincent Kigosi ‘Ray’ amefika kwenye penzi lake ndiyo maana ametulia
kwani amepata ‘malovee’ aliyokuwa akiyatafuta siku zote.
Staa huyo alisema hivi sasa Ray hafurukuti kwake kwani anampa mapenzi motomoto. “Hapa Ray amefika aambiwi kitu,” alisema Chuchu.Alipoulizwa sababu ya kusherehekea hospitalini hapo aliweka wazi kuwa ilitokana na yeye kuzaliwa ‘premature’ na mwanaye kumzaa akiwa ni premature hivyo aliona awakumbuke watoto wa aina hiyo na waliozaliwa na kufiwa na wazazi wao huku wakiwa wodini.
Chuchu aliyeongozana na wasanii kadhaa, aliwapatia watoto hao zawadi mbalimbali.






