FAMILIA YA STEENKAMP YAPINGA UAMUZI, SOMA ZAIDI HABARI HII HAPA

Wanafamilia kutoka upande wa marehemu Reeva wakiwa na simanzi wakati wa hukumu hiyo.
Familia ya Reeva Steenkamp ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi na mwanariadha wa Afrika kusini Oscar Pistorius imekasirishwa na uamuzi wa jaji wa kesi hiyo baada ya kumpata na hatia ya mauaji ya kutokusudia na kumuondoalea mashtaka ya mauaji.
Jaji Thokozile Masipa alisema kuwa mwanariadha huyo alimuua Reeva kwa bahati mbaya.
June Steenkamp amesema kuwa mwanawe ambaye alikufa vibaya hakufanyiwa haki.
Amesema kuwa hakuamini kwamba jaji wa kesi hiyo alikubali ushahidi wa Oscar Pistorius kwamba alidhani bi Reeva Steenkamp alikuwa mtu ambaye alikuwa amevamia nyumba yao.

Oscar Pistorius akisikiliza hukumu yake.
Hatahivyo mjombaake Pistorius alimshukuru jaji huyo kwa kumuondolea mashtaka ya mauaji mwanariadha huyo.
Oscar Pistorius ataendelea kuwa nje kwa dhamana hadi hukumu yake itakapotolewa mnamo mwezi ujao.

Baba mzazi wa Oscar, Henke Pistorius akifuatilia kwa makini hukumu ya kijana wake.
(CREDIT: BBC)