MAMA ABDUL AWAPONDA WANAOIBA KWENYE MISIBA

STAA wa filamu ya Kigodoro, Mama Abdul ‘Kantangaze’ hivi karibuni alitoa kali ya mwaka baada ya kuwacharukia wezi wa nyama misibani, hasa akina mama.

Staa wa filamu ya Kigodoro, Mama Abdul ‘Kantangaze’.
Mama Abdul alitoa kauli hiyo baada ya kuwaona akina mama wakidokoa nyama kwenye sahani za vyakula zilipokuwa zikipitishwa wakati wa msiba wa Mc Chimamy, eneo la Sinza jijini Dar es Salaam.
“Mnanisikitisha sana akina mama, hizi nyama mnazoiba leo, ipo siku nanyi mtaibiwa kwenye misiba yenu, kuweni na utu, nyama kitu gani watu tunalia nyie mnaiba nyama” aliwananga Mama Abdul.