MSANII nyota wa filamu za
kibongo, Jennifer Kyaka maarufu kwa jina la kisanii kama Odama, usiku wa
kuamkia Jumapili iliyopita alinaswa Live akiwa kwenye pozi la aina yake
akiwa na pedeshee maarufu jijini Dar anayefahamika kama Papaa Daudi
ambaye anadaiwa kuwa mume wa mtu.
Wakiwa ukumbini humo, wawili hao walionekana kupata kiburudisho kwa namna yake huku mara kwa mara wakigonga ‘chiaz’ na kunyweshana mvinyo na kuwafanya waliokuwa karibu yao kuwaonea gere.
Licha ya macho ya watu kuonekana kuwatazama kwa muda mwingi, lakini wawili hao hawakumjali mtu bali waliendelea kuponda raha huku mikono ya mwanaume ikiwa haichezi mbali mapajani mwa Odama.
Baada ya kupata picha kadhaa za wawili
hao, Paparazi wetu aliwasogelea na kuwauliza kama wao ni mtu na mwenza
wake, lakini wakabeza na kumtaka awaache wale raha zao.
Msanii nyota wa filamu za kibongo, Jennifer Kyaka.
“Aaaah jamani hebu tuacheni jamani nyinyi kila mkiona watu
wanastarehe, mnaanza kuhisi ni wapenzi, hebu tuacheni jamani,” aliongea
Odama huku akipata mvinyo.Papaa Daudi alipotakiwa kutoa neno, alisema:
“Nakuomba sana, we ndugu mwandishi, ntafute siku nyingine leo hatuna
muda.”






